UNITED KUVUNJA REKODI KWA SNEIJDER



Masaa machache baada ya Gary Neville kusema anaamini Wesley Sneijder atajiunga na United, pamoja na Sir Alex Ferguson kuonekana kujitoa katika mbio za kumsaini Samir Nasri, habari kutoka mtu wa ndani wa United na baadhi ya wachezaji wamekaririwa na gazeti la The Sun kuwa The Red Devils wapo tayari kutuma ofa ya £35million ambayo ni rekodi kwa klabu ili kuweza kumsaini Wesley Sneijder .
Moja ya wachezaji United alikaririwa akisema: “Kila mtu anafahamu juu ya harakati za usajili wa Sneijder kuja United, na anategemewa kutangazwa mapema sana kuwa mchezaji mpya wa United, kuanzia Jumatano wiki hii.”
Inter Milan wanahitaji cash ili waweze kusajili na mtu pekee anayeweza kuingiza fedha ya kutosha ni Sneijder.
“Sneijder ameshaongea na Nigel De Jong kuhusu mahali pazuri kwa kuishi ndani ya jiji la Manchester.Inter na Wesley wanaweza kuongea chochote mbele ya jamii lakini ukweli ni kwamba timu inataka kumuuza lakini wanshindwa kukiri, mchezaji anataka kuondoka lakini hataki kusema kwa kuogopa kukera mashabiki wake.Hii ni hatua nzuri na biashara nzuri kwa timu,”-kiliongea chanzo cha habari.

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item