MECHI YA WABUNGE WA SIMBA NA YANGA: WABUNGE WA SIMBA WATAJA KIKOSI CHA KWANZA CHA MAANGAMIZI

HOMA ya pambano la Wabunge wa timu ya Simba dhidi ya watani wao wa Yanga imezidi kupanda ambapo sasa kikosi cha wekundu hao kimetaja jeshi kamili litakalopeleka ushindi katika kambi yao.
Pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa michezo nchini linatarajiwa kufanyika Julai 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati wa Tamasha la Matumaini.
Nahodha wa kikosi cha Simba, Amos Makalla amesema tayari timu yao imeshapata kikosi cha kwanza kitakachopeleka majonzi kwa watani wao ambapo langoni kutakuwa na Idd Azzan, wakati mabeki wakiwa ni Yusuph Masauni, Yona Kirumbe, William Ngeleja na Kizingiti wakati viungo watakuwa Adam Malima, Kingwangala na yeye mwenyewe (Makalla).
Makalla alisema kuwa safu ya ushambuliaji itaongozwa na Joshua Nassari akisaidiana na Zitto Kabwe na Juma Nkamia, amedai kuwa tayari kikosi chao kimepata daktari mkuu ambaye ni Cosmas Kapinga anayetoa huduma hiyo na kikosi chao halisi cha klabu ya Simba.
vipi habari hii: 

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Follow by Email

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item