Page

Friday, January 4, 2013

JOHN MNYIKA AWAKILISHA MUSWAADA BINAFSI

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Jijini Dar es salaam, nchini Tanzania JOHN MNYIKA, amewasilisha kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Muswaada binafsi wa Sheria ya Kuundwa kwa Baraza la Taifa la Vijana litakalowawezesha kujadili na kuamua masuala ya kisera na Kisheria yanayogusa maslahi yao.
MNYIKA amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na Serikali kushindwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda Baraza hilo kwa Kipindi cha zaidi ya Miaka kumi hali inayosababisha Vijana nchini kushindwa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Ameongeza kuwa Mswaada huo umegawanyika katika sehemu nane ikiwemo ile ya kupendekeza kuanzishwa kwa Majukwaa ya Vijana katika ngazi ya Halmashauri, na Kamati za Vijana za Kata, Vijiji na Mitaa kwa madhumuni ya kuzishusha Chini shughuli za Vijana.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA