Page

Sunday, October 20, 2013

BODABODA FC YAIBAMIZA MAPEA FC: MAGUGU

Katika michuano ya kumtafuta Bingwa wa kombe la Mbuzi hapa Magugu Manyara, leo kumeshuhudiwa kimbembe kati ya Bodaboda Fc na Mapea. Katika mtanange huo, Mshambuliaji machachali kutoka Bodaboda Fc, Yona a.k.a Bonge aliifungia timu yake magoli mawili na kuipa point Tatu muhimu. Hadi sasa Bonge ndio ni kinara wa magoli kwa kupachika magoli matano mpaka sasa. Bodaboda ilishinda goli 2-0. Michuano hiyo itaendelea kesho.

Mwenye jezi nyekundu ndio BONGE

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA