Micho ampa Kaseja siri nzito za Wydad

J. Kaseja mchezaji wa simba.
KOCHA wa Al Hilal ya Sudan, Sredejovic Milutin 'Micho' ametoa siri za wachezaji watatu wa Wydad Casablanca ya Morocco na akamuonya kipa wa Simba, Juma Kaseja.

Micho, ambaye amewahi kuwa kocha wa Yanga, alisema kutoka mjini Khartoum jana Jumatatu kuwa, Wydad hufunga mabao mengi kwa mipira ya 'free kick' na kona na kwamba ni wazuri kwa mipira ya juu ambayo hupotezwa na wapinzani.

"Ninawajua vizuri sana, ni timu ambayo mara zote hutafuta faulo ili wakufunge kwa jinsi hiyo. Ni wazuri sana kwa kupiga 'free kick', kona na mipira ya juu," alisema Micho, ambaye amewahi kuifundisha Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Micho akaenda mbali zaidi kwa kuwataja wachezaji watatu wa Waydad Casablanca ambao ni Mustapha Allaoui aliyekuwa anacheza Ufaransa, Fabrice Ondama wa Congo Brazzaville na Pascal Angan wa Benin kuwa ndizo mashine ambazo zinapaswa kuchungwa sana na Simba kwani ni hatari tupu.

"Wachezaji hao hucheza kwa ushirikiano mkubwa na kwa mfumo wa sambusa (pembe tatu) ni hatari sana, hasa huyo Mustapha Allaoui, ambaye hucheza timu ya taifa ya Morocco," alisema Micho.

Micho alisema kipa na mabeki wa Simba wanatakiwa kuwa makini sana na hasa wakati wa faulo au kona zinapopigwa kuelekea katika lango lao.

"Kuna vitu viwili; kona na faulo, waambie Simba kuwa makini kwa sababu wachezaji wa Wydad huzitafuta kwa nguvu na huwa wanafunga," alisema.

Micho aliwataka Simba kucheza mpira wa chini zaidi kwani Wydad Casablanca ni wazuri kwa mipira ya juu na huwa wanahakikisha wanaiwahi mipira iliyopotea.

"Simba wacheze mpira wa chini. Wachezaji wengi wa Afrika Kaskazini si wazuri kwa mipira ya chini kwa sababu ya miili yao. Mabeki wao wanacheza taratibu, ninaamini kasi ya Emmanuel Okwi na wenzake inaweza kuwamaliza. Lakini Simba wasipoteze pasi, jamaa wale ni hatari sana kwa mipira inayopotea," alisema kocha huyo wa Serbia.

"Halafu wanapenda sana kutumia mipira mirefu na kuifanya beki ya wapinzani kuwa na wakati mgumu. Kama Simba wanataka kuwadhibiti wanatakiwa kuhakikisha wanaziba mianya yote. Wasiwaache wacheze mpira wao, watawamaliza.
"Lakini Simba nao wanatakiwa kushambulia kwa akili na si kupanda mbele bila mpango wowote," alisema kocha huyo wa zamani wa SC Villa ya Uganda.

Micho alisema faida waliyonayo Simba ni kwamba mabeki wa Wydad Casabalanca hucheza taratibu sana na hilo linaweza kumfanya Emmanuel Okwi na Mussa Hassan 'Mgosi' kupata mwanya wa kufunga mabao.

Simba itacheza na Wydad Casablanca Jumamosi mjini Cairo, Misri saa 12:00 jioni katika mchezo ambao utaamua timu ya kucheza Nane Bora pamoja na Al Ahly ya Misri, MC Algers ya Algeria na Esperance ya Tunisia katika Kundi B.

Related

free to all 1533101082606845872

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item