WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2014 WATANGAZWA

Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule za Serikali..Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.

Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.hadi ifikapo machi mwaka mwakani..Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi.waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 412.

Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.

Related

Education 6276367572266627136

Post a Comment

1 comment

Unknown said...

Mbona hamja onesha matokeo ya darasa la saba 2013 walio chaguliwa kwenda kidato cha kwanza wakati hapo mmeandika walio chaguliwa then ukicheki unakuta ni maelezo tu

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item