AJIRA 26 ,000 ZA WALIMU KUTOLEWA JAN, 2014
SERIKALI imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifunga kikao cha kazi cha siku tatu cha maofisa elimu wa mikoa na.halmashauri za wilaya nchini,.wanaosimamia elimu ya msingi. “Serikali inatambua uhaba wa walimu na. kila mwaka inatoa ajira mpya za walimu. Januari 2014 Serikali itatoa ajira 26,000 za walimu wapya na maelekezo mengine yatafuata,“ alisema Majaliwa.
Aliwataka maofisa elimu hao kuzingatia uwiano wa walimu wakati wa kuwapangia vituo vya kazi, badala ya kuendelea.kuwalundika maeneo ya shule za mijini pekee. Pia aliagiza walimu hao watayarishiwe mazingira mazuri hasa katika maeneo ya.pembezoni kwa kuwapatia motisha, ili.kuwajengea moyo wa kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi katika vituo vyao vya kazi kwa lengo la kuwafanya.wasikimbie vituo. Licha ya kutangaza ajira hizo mpya,
Majaliwa pia alisema Serikali imetenga Sh bilioni 18 za kutengeneza madawati
yatakayosambazwa shuleni na zabuni yake inatarajiwa kutangazwa mapema
iwezekanavyo. Alisema mpango huo unatarajia kuanza mapema mwakani baada ya kumpata mzabuni, “najua kutokana na kiwango kidogo cha fedha, hatutaweza kutosheleza, lakini huu ni mwanzo.” Aliwataka maofisa hao kujenga tabia ya ufuatiliaji shuleni, ili kusimamia utunzaji wa vifaa na wakikuta uzembe ni wajibu wao kuchukua hatua ya kumaliza matatizo yaliyo chini na uwezo wao.
CHANZO: HABARI LEO 23/12/2013
Post a Comment