CHOMBEZO: GUBERI LA KIMANYEMA
https://menacotz.blogspot.com/2012/12/chombezo-guberi-la-kimanyema.html
MTUNZI: INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
SIMU: 0713 59 35 46/0755 04 05 20
Sharifa alilainika kama mboga ya bamia. Akakamatwa kiuno na kuvutiwa
kwenye kitanda cha mama yake. Wakashiriki dhahama. Naam, hawakujua ni
ngoma ipi waliyocheza pale kitandani. Kama ni sindimba, basi ilikuwa
sindimba kweli. Kama ni Mduara basi ulikuwa ni Mduara halisi. Kama ni
Mugongomugongo, ilitisha. Chumbani kwa Mama Kadala, kitandani kwa Mama
Kadala, na mtoto wa Mama Kadala!
Kiwembe! Kabalehe kwenye kifua cha
Mama Kadala, na sasa anafanya mazoezi kwenye mwili wa mtoto wa Mama
Kadala! Kwenye kitanda kilekile!
Huo ulikuwa ni mwanzo tu, mwanzo
uliofungua ukurasa mpya wa uhusiano baina yao. Penzi likawanogea. Awali
ilikuwa ni siri, siri iliyofichika, lakini hatimaye minong’ono ikaanza
kuzagaa mitaani. Siri hiyo ilianza kufichuka.
“Kiwembe anachukua mama na mtoto…!” watu walinong’ona.
Walinong’ona lakini haikuwa ni minong’ono iliyokuwa na mipaka maalum.
Hapana. Iliyafikia masikio ya watu tofauti, na hatimaye Mama Kadala
akaipata. Hakukubali kupuuzia taarifa hizo. Alimjua bintiye jinsi alivyo
na mvuto mkali katika sura na umbo lake. Ni rijali gani
atakayestahimili kutomtamkia neno lihusulo mapenzi endapo watakuwa na
wasaa wa kuwa pamoja kwa muda mrefu?
Ndipo akaamua kufanya
uchunguzi wa kina, taratibu na kwa siri kubwa. Hakutaka kumshirikisha
mtu yeyote katika uchunguzi huo. Hatimaye, siku ya siku akashuhudia kwa
macho, Kiwembe na Sharifa wakiwa kitandani kwake, mchana kweupe!
Alichokiona hapo, hakivumiliki wala hakisemeki. Kwanza alihisi yu
ndotoni, akiota ndoto isiyopendeza. Hatimaye akazinduka na kubaini kuwa
anachokishuhudia mbele yake si ndoto wala tamthiliya bali ni tukio
halisi, tukio ambalo halikutofautiana na maumivu ya kisu chenye moto
kikipenya kifuani mwake.
Chozi likamtoka Mama Kadala. Chozi lenye
tani kadhaa za uchungu nyuma yake. Kwa ujumla hakutegemea kuwa kijana
yule aliyebalehe kifuani pake, leo atokee kuwa mpenzi wa mwanae,
Sharifa, wakidiriki kuchojoa nguo na kukitumia kitanda chake kwa starehe
zao.
Mama Kadala alisononeka, uvumilivu ukamshinda, akaamua kupasulia ukweli Kiwembe.
“Nakuapia kijana wewe, kama hukubalehe kwenye maungo yangu haya,
utaendelea kuwa kichaa wa mapenzi bila ya kudhurika. Lakini kama
umebalehe hapa maungoni mwangu, halafu eti unamrudi binti yangu, wallahi
nakuapia, janga litakupata katika huo wendawazimu wako.”
Wakati
Mama Kadala akiongea hayo, alikwishavua nguo zote, yuko mtupu kama
alivyozaliwa, machozi yakiendelea kububujika mashavuni, akimwonyesha
Kiwembe kile kilichomfanya mtoto huyo akawa kichaa wa mapenzi.
Siku
hiyo, saa hiyo na dakika hiyo ukawa mwisho wao wa kujuana. Kiwembe
aliondoka kwa Mama Kadala kama alivyoingia. Akawa mtoto wa mitaani,
mtoto asiyejali mambo ya kwenda shule wala kujitafutia riziki kwa kusaka
vibarua huku na kule. Zaidi alikuwa akivizia tu kupata mlo kwa mama
yake mdogo, ambaye kama kawaida yake aliendelea kutomjali.
Kwa
jinsi kitongoji cha Ujiji kilivyokuwa kidogo, Kiwembe angeweza
kukimaliza kimapenzi. Hata wake za watu ambao wangeingia kwenye ‘anga’
zake asingewachekea. Aliwaza mapenzi tu, na kila mwanamke mzuri
aliyemtia machoni alitamani awe mpenzi wake.
Pumzi yake, mapenzi!
Shibe yake, mapenzi!
Lakini, pamoja na hayo, maneno makali ya Mama Kadala yalielea kichwani
mwake bila ya kukoma, yakamfadhaisha na kumtia hofu. Akakiona
kitongoji hicho kikiwa hakitofautiani na Jehanamu. Akahamia kitongoji
cha Mwanga, mtaa wa Kitambwe kinyemela.
SOMA STORI KAMILI HAPA>>>>>>>>>>>>>>
Post a Comment