WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2014 WATANGAZWA

Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule za Serikali..Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.

Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.hadi ifikapo machi mwaka mwakani..Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi.waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 412.

Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.

Related

BREAKING NEWZZZ: MATOKEO KIDATO CHA SITA 2014 OUT, YAANGALIE HAPA

Matokeo ya kidato cha sita yametoka, kama una ndugu au jamaa au wewe mwneyewe ulifanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu basi ingia hapa na uyaone matokeo yako mwenyewe pia wajulishe na wengine&...

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA!

Majira ya saa nane mchana siku ya leo, hatimaye matokeo ya kidato cha nne 2013 yametangazwa baada ya kusubiriwa kwa hamu na wadau kwa muda mrefu sana. Jedwali hili hapa chini ni summary tu ya matokeo...

AJIRA 26 ,000 ZA WALIMU KUTOLEWA JAN, 2014

SERIKALI imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini. Naibu Waziri wa Nchi, O...

Post a Comment

1 comment

Unknown said...

Mbona hamja onesha matokeo ya darasa la saba 2013 walio chaguliwa kwenda kidato cha kwanza wakati hapo mmeandika walio chaguliwa then ukicheki unakuta ni maelezo tu

ads by blogger

Follow Us

Hot in weekRecentBLOG ZINGINE

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item