SIMULIZI YA KWELI::: KAMA UNAMACHOZI YA KARIBU USISOME..!! SIMULIZI YA KWELI YA KUSISIMUA NA KUSIKITISHA YA MTOTO JANETH..!!


Kengele ya kutoka darasani iligongwa,
wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza kutoka
madarasani huku wakifukuzana wengine
wakipiga kelele ilimradi shwangwe tu.
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufundisha
shule za hatua hiyo.
Ilikuwa ni shule ya serikali.
Jicho langu liliangukia katika sura ya msichana
mdogo, nguo zake chafu. Alikuwa analia.
Alikuwa peke yake na hakuwa na yeyote wa
kumbembeleza.
Mimi kama mwalimu sikutaka kujisogeza karibu
naye sana. Kwanza nilikuwa mgeni.
Nikaachana naye.
Siku iliyofuata tukio kama lile likajirudia.
Msichana yuleyule wakati ule uleule wa
kutawanyika, alikuwa analia sana. Mwishowe
aliondoka huku akiwa analia.
“Mbona mwenzenu analia?” nilimuuliza
mwanafunzi mmoja.
“Huyo ni mama kulialia..” alinijibu huku
anacheka.
Haikuniingia akilini hata kidogo kuwa yule binti
analia bila sababu.
Siku ya tatu nikaanza kujiweka karibu naye.
Muda wa mapumziko nilimwita nikamnunulia
chai, alikuwa ananiogopa na hakutaka
kuniangalia machoni.
Sikumuuliza lolote juu ya tabia yake ya kulia lia
kila anaporuhusiwa kurejea nyumbani.
Hata siku hiyo pia alilia vilevile. Wenzake
wakawa wanamzomea.
Akili yangu iligoma kuamini kuwa binti yule
analia bila sababu.
Kwanini alie wakati wa kutawanyika tu??
Hapana si bure.
Nikaendelea kujiweka karibu naye. Mkuu wa
shule akafikishiwa taarifa kuwa nina mahusiano
ya kimapenzi na yule mtoto.
Moyo wangu na Mungu pekee ndio walikuwa
mashahidi. Nilikosa cha kujibu.
Nilijaribu kujiweka mbali naye lakini moyo
ulinambia kuwa kuna jambo natakiwa kulijua.
Nikaendelea kuwa karibu naye. Hatimaye mkuu
wa shule akanisimamisha kufundisha pale kwa
tabia yangu ya kufanya mapenzi na
mwanafunzi.
Nilijitetea lakini sikueleweka. Nikamwachia
Mungu……
Licha ya kusimamishwa kazi, niliendelea
kufuatilia nyendo za yule binti aliyeitwa Janeth.
Kila alipotoka shule nilimvizia njiani na
kumnunulia chakula, kisha tunazungumza
kidogo.
Aliponiamini kama kaka yake ndipo nikajieleza
dukuduku langu.
“Janeth…” nilimuita.
“Bee kaka ….” Aliitika huku akinitazama.
“Nyumbani unaishi na wazazi.”
“Ndio naishi na mama..baba huwa anasafiri
safari.”
“Mama yako ana watoto wangapi?”
“Mama yangu alikufa….alikufa nikiwa mdogo
hata simkumbuki” Alijibu kwa sauti ya chini.
“Kwa hiyo unaishi na mama mdogo.”
“Ndio.”
“Unampenda mama mdogo?”
Swali hili likaikatisha furaha ya Janeth. Akaanza
kulia, alilia bila kukoma, Janeth alilia kwa
uchungu hadi nikajisikia vibaya. Nilimbembeleza
kisha sikumuuliza tena.
Siku zikaenda bila kumuuliza chochote..
Baada ya siku kumi, ilikuwa siku ya michezo
pale shuleni, hivyo hapakuwa na masomo.
Janeth alichelewa kuja shule, nilimngoja
uwanjani, hadi alipofika majira ya saa nne.
Nikamwambia twende kunywa chai.
Siku hiyo nilimpeleka mbali kidogo, tukanywa
chai, kisha tukakaa mahali palipokuwa wazi.
Nikaleta tena mjadala mezani.
Ni kuhusu maisha ya Janeth.
Alikataa kabisa kusema lolote, nilimshawishi
sana.
“Usiogope mimi ni kaka yako.” Nilimpooza.
Janeth badala ya kusimulia akaanza kulia tena.
“Ataniua mama nikisemaaaa” alilalamika.
Nikambembeleza hatimaye akanieleza jinsi
anavyonyanyaswa na mama yake.
“Mama hanipendi hata kidogo, ananipiga na
kuninyima chakula, hapendi nije shule, vyombo
tunavyotumia usiku hataki nivioshe usiku na
hataki niwahi kuamka asubuhi, nikiamka
natakiwa kufanya kazi zote, kufagia uwanja,
kudeki nyumba, kuosha vyombo kisha ndipo
nije shule. Baba akiwepo anajidai kunijali
sana…”
Alijieleza.
“Ni hayo tu Janeth….niambie kila kitu.”
“Akijua ananiua alisema….”
“Kwani amewahi kukutesa vipi..”
Ni hapa Janeth alivyozungumza huku analia kilio
ambacho hakitatoka masikioni mwangu kamwe.
Siku moja, alichelewa kuamka, ilikuwa siku ya
mapumziko.
Mama yake alipomwamsha, aliitika na kupitiwa
usingizi tena.
Mama aliporejea mara ya pili, alikuwa na mti
mkavu, alimpiga nao kichwani na popote pale
katika mwili, alipoona hiyo haitoshi akamvua
nguo, akausokomeza katika sehemu za siri,
aliuigiza hovyohovyo, ukuni huo ulikuwa wa
moto.
Yeyote mwenye moyo wa nyama ajifikirie ukuni
wa moto ukazamishwa sehemu za siri za mtoto
wa darasa la sita.
Nilitokwa machozi.
Nikawahi kujifuta hakuona.
“Baba yeye alisemaje….”
“Baba ni mkali na hapendi kunisikiliza na mama
aliniambia nikiambia mtu ananiua mara moja.”
Alijibu kwa huzuni.
“Nikija na dada yangu tunaweza kukuona
ulivyounguzwa..”
“Ndio…” alinijibu.
Sikutaka kulaza damu nikampigia simu rafiki
yangu wa kike.
Nikamuuliza kama yupo kwake, alikuwepo.
Nikaongozana na Janeth.
Tukafika, Janeth akatoa nguo zote.
Ilihitaji moyo wa kiuaji sana kutazama mwili wa
Janeth mara mbilimbili.
Alitisha, hakika alikuwa ameunguzwa vibaya na
vidonda vilikuwa havijapona vizuri.
Dada yule alishindwa kujizuia alimlazimisha
Janeth twende kwa mama yake amkabiri na
kumpa kipigo. Nikamzuia.
Hata mimi nilikuwa na hasira kali. Lakini
sikutaka kuiruhusu ifanye kazi.
Nikachukua kamera, nikampiga picha Janeth
katika yale makovu.
Mbio mbio nikaenda polisi, kituo cha haki za
watoto nikaelezea mkasa ule huku nikishindwa
kujizuia machozi.
Nikawaonyesha na picha.
Tukaongozana nao hadi nyumbani kwao Janeth.
Mama yule akakamatwa bila kutarajia.
Nilitamani kumrukia nimng’ate lakini
haikuruhusiwa.
Sheria ikafuata mkondo. Janeth akaanza
kupokea tiba.
Yule mama akahukumiwa kwenda jela miaka
sita..hadi sasa yupo jela.
Mume wake alitozwa faini kubwa kwa kosa la
kutofuatilia maendeleo ya mtoto wake
kiafya……..
Mimi nilirudishwa kazini, kwa heshima kubwa.
Heshima ya nkumkomboa mtoto.
***Akina JANETH wapo mtaani
kwako…..usiwaangalie na kuwaacha tu…hebu
jaribu KUWA SAUTI YAO… .hawawezi kusema…
hebu sema badala yao…….wanalia kisikie kilio
chao…….
KAMA UMEGUSWA NA MKASA HUU SHARE NA
NDUGU JAMAA NA
MARAFIKI ZAKO ILI WAONE

Related

HADITHI 4409868376963286897

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item