bajeti ya elimu yaongezwa ni asilimia 12 zaidi

vyuo vikuu vya tengewa sehemu kubwa zaidi
lengo ni kuopunguza makali ya maisha 

na sir meja

SERIKALI imefanya marekebisho katika mgawanyo wa mapato yatokanayo na tozo ya kuendeleza ufundi stadi ya asilimia sita ili asilimia nne zipelekwe kwenye bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Akiwasilisha Bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12 bungeni  jana, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo alisema  asilimia mbili zitapelekwa  mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (Veta) na kwamba lengo la hatua hii ni kuongeza fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

“Hatua hii katika elimu na mafunzo ya ufundi stadi haijatarajiwi kupunguza wala kuongeza mapato ya serikali,”alisema Waziri Mkulo.Alisema wizara ya elimu imetengewa Sh 2,283 bilioni  ikilinganishwa na Sh 2,045 bilioni za mwaka 2010/11 na kwamba hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 12.

Alisema ongezeko la asilimia 12 huenda likaleta nafuu katika sekta ya elimu ambayo inakabiliwa na matatizo lukuki.Waziri Mkulo alisema watalinda na kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta za huduma za jamii hususan elimu, maji na afya .

Hata hivyo sekta ya elimu ndio yenye  wadau wengi wanaoitegemea kutokana na Watanzania takribani milioni 40 kupitia katika sekta hiyo.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekuwa na misukosuko mingi hapa nchini na ndio msimamizi mkuu wa elimu, lakini kadri muda unavyokwenda  maendeleo ya elimu yanakabiliana na changamoto nyingi.

Mpaka sasa wanafunzi wa shule nyingi hapa nchini  wanasoma wakiwa wamekaa chini kutokana na ukosefu wa madawati hali ambayo wataalamu wa elimu wanasema inachangia wanafunzi kushindwa mitihani yao.

Hali kadhalika walimu wanakabiliwa na kero nyingi zikiwemo za kukosa nyumba za kuishi, kukosa mishahara baada ya kuajiriwa.

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item