LEO BAJETI YA TANZANIA KWA MWAKA WA FEDHA 2011/12
https://menacotz.blogspot.com/2011/06/leo-bajeti-ya-tanzania-kwa-mwaka-wa.html
hii ni bajeti ya mwaka jana
leo watanzania wote macho yao yatakuwa bungeni wakati wakusomwa bajeti ya fedha kwa mwaka wa fedha 2011/12. hata hivyo leo bungeni mh. m.mkulo wakati anasoma tathmini ya uchumi kwa mwaka jana alieleza baadhi ya vipa umbele kwenye bajeti ya leo kuwa ni
1.nishati ya umeme
2.viwanda
3. kilimo
hivyo ni baadhi ya vipa umbele ambavyo tunategemea kama alivyosema kuona vikiwa katika bajeti hii ya mwaka wa fedha. hata hivyo bajeti hii imekuja wakti maisha ya watanzania wengi yakiwa magumu hususani kupanda kwa bei ya vyakula, umeme, mafuta na ajira kwa vijana likiwa ni tatizo kubwa sana kwa sasa.
hata hivyo wakati akisoma taarifa ya hali ya uchumi wa nchi kwa sasa mh.mkulo alisema baadhi ya vitu vinavyo sababisha umasikini kwa waafrika na tanzania ikiwemo ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana
na kikundi kikubwa ambacho kina isubiri bajeti hiyo kwa makini ukiwaacha wafanyakazi na wakulima ni pamoja na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kwani matukio mengi ya kuandamana katika vyuo vikuu yanasababishwa na hela ndogo wanayopewa wanafunzi hao muhimu hapa tanzania. swali ni je booooom litaongezeka?
Post a Comment