wanafunzi wafariki Main Compus Mwanza- SAUT


Na Jelard Lucas Mwanza
HOFU na simanzi imetawala na kutikisa wanajumuiya ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, (SAUT) Mwanza baada ya kutokea misiba ya wanafunzi wanne wa kitivo kimoja kwa nyakati tofauti.

Kilichosababisha hofu kwa wanajamii hao  ni kutokana na wanafunzi hao wa Kitivo cha Elimu, John Richard, Ngaiza Joseph, Kadome Andrew  na John Shango kufariki dunia mfululizo ndani ya mwezi mmoja, kati ya Mei 22 na Juni 22, mwaka huu.

Baadhi ya wanachuo waliozungumza na mwandishi wa habari hii ambao waliomba majina yao kutoandikwa gazetini, walisema vifo hivyo vinafanya wajiulize maswali bila kupata majibu.

“Kwa mfano John alifariki dunia baada ya kuomba ruhusa ya kwenda nyumbani kwao kufuatia kupata taarifa ya msiba wa baba yake mzazi, lakini wakiwa kwenye gari na rafiki zake walipofika Nzega gari lilipinduka na akafariki palepale na alizikwa siku moja na baba yake,” alisema mwanafunzi mmoja.

Aliongeza kuwa kifo cha mwanafunzi huyo walitaarifiwa na  Mama Mlezi wa wanachuo, Scholastica Nasania ambaye alitoa tangazo kwenye ubao wa matangazo wa chuo.

Awali kabla ya kicho hicho, jamii hiyo ya chuo hicho ilipata pigo baada ya mwanafunzi mwingine, Josephat kufariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mei 22, mwaka huu baada ya kuugua kile kilielezwa mapafu.
Mwili wa marehemu Ngaiza uliagwa na wanafunzi wenzake katika hospitali hiyo na kusafirishwa kwenda Bukoba kwa mazishi Mei 23, 2011.

Hata hivyo, kabla ya jamii hiyo ya chuo haijasahau misiba hiyo, ilipata pigo tena Juni Mosi mwaka huu baada ya mwanafunzi mwingine, Shango kufariki dunia.

Aidha, Jumapili iliyopita uongozi wa chuo ulitoa taarifa ya kifo cha  Kadome Andrew, mwanafuzi kutoka kitivo hicho hicho cha elimu, aliyefariki dunia Juni 4, mwaka huu  akiwa  nyumbani kwao Nzega,Tabora kwa kile kilichoelezwa kuwa aliugua ini.

Japokuwa wasomi wengi hawakubaliani na mambo ya kishirikina, lakini baadhi ya wanajamii walio karibu na chuo hicho na hata wasomi wenyewe wanajiuliza kwa nini  vifo vinatokea kwenye kitivo kimoja.

Hata hivyo,  Waziri wa Michezo wa SAUT, Jackson Kadutu alipohojiwa kuhusiana na misiba hiyo alisema: “Vifo ni jambo la kawaida lakini vinapotokea mfululizo kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa inauma sana pia mimi binafsi nimegubikwa na simanzi.” Aidha, hivi karibuni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Dk. Charles Kitima ambaye pia ni mchungaji, aliwaombea dua njema wanafunzi wote wanne waliofariki dunia katika Uwanja wa Raila Odinga chuoni hapo.

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item