SABODO Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania


MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffer Sabodo, amesema hajahama na wala hana mpango wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho amekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40.

Sabodo alisema baadhi ya kauli kali ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya CCM, hazina maana kuwa anaichukia, isipokuwa zinalenga kukikosoa Chama ili kiendelee kuwa imara katika kuwaongoza Watanzania na kuharakisha maendeleo yao. Hayo aliyasema jana alipozungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati nyumbani kwake, Upanga, Dar es Salaam na kuwataka wana CCM na wananchi kwa jumla wasimwelewe vibaya.

"Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, “Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi.”
Alitoa toa wito kwa wananchi kutofanya makosa ya kufanya majaribio ya kuwapa ridhaa wapinzani kuunda serikali. "Nawaomba Watanzania wenzangu, tusifanye majaribio ya kuwapa CHADEMA au chama kingine chochote zaidi ya CCM kuongoza serikali kwa kuwa havina uzoefu, hatuwezi kufanya majaribio ya kuliweka rehani Taifa," alisema mfanyabiashara huyo.

SOURCE: JAMIIFOR

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item