ACADEMIC NEWZ: Profesa Mukandala awapa somo wahitimu UDSM

Dar es Salaam

WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wametakiwa kutumia taaluma zao katika kuikomboa nchi, pamoja na kujikwamua wao wenyewe kiuchumi. Akizungumza mwishoni mwa wiki chuoni hapo, katika mahafali ya 42, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema elimu waliyoipata wahitimu hao, itumike kuwakwamua wao binafsi pamoja na nchi kwa ujumla, kwani wametumia kodi za wananchi kupata elimu hiyo. "Sisi kama viongozi tumefurahi kwa hatua hii ambayo mmeifikia leo, lakini tunawashauri, kwamba msibweteke, endeleeni kusonga mbele zaidi na mtumie taaluma yenu kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla," alisema Mukandala. Mukandala alisema, uongozi wa chuo hicho umeandaa dira ya nusu karne ijayo, ambapo ifikapo mwaka 2061, watakuwa wanatoa elimu bora yenye viwango vya kimataifa, kwa kuwa lengo ni kukifanya chuo hicho kiwe kinara wa utoaji elimu ya juu yenye ubora duniani.
SOMA HABARIAKILI HAPA >>>>>>>>>>>>>>>>>>

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item