CHOZI LA FUKARA
https://menacotz.blogspot.com/2012/10/chozi-la-fukara.html
NA DEARNA MAROTA
Mungu mwenyezi ni mkuu aliyeweza kuwaumba
binadamu kwa mfano wake lakini kwa wepesi na ugumu wa nafsi tofauti tofauti.
Mwanadamu huweza kutoa chozi lake
kwa hisia tofauti: -
machozi ya furaha na machozi ya uchungu. Chozi litokalo kwa uchungu wa jambo
fulani huwa ni pigo lililo na pengo ndani ya moyo wa mwanadamu, CHOZI LA FUKARA ni story ambayo inaelezea jinsi masikini anavyo nyanyaswa na
penzi kutokana na UFUKARA wake, na
kujihisi hana nafasi ya kueleza hisia zake kwa mtu ampendaye kutokana na
umasikini wake.
“mwanzo wa mapenzi huwa matamu zaidi ya
asali na mwisho wa kulishamirisha huwa kama shubiri iliyotiwa pilipili kichaa
iliyo mbichi haswaaaa, kwa fukara kama mimi kwani penzi limeweza kunitoa chozi
na pia kuninyanyasa katika nafsi yangu pia nikatambua fukara hana sauti” maneno
haya yalitoka kinywani mwa Jordan ambaye ni kijana apatae miaka 30 kwa sasa na
anafamilia hivyo ameamua kuelezea mikasa ya maisha yake na misukosuko ya
mapenzi aliyopitia pindi alipokuwa masikini lakini mungu alikuwa pamoja nae mpaka
kufikia hapo alipo sasa ndipo anaelezea kwa uchungu huku akivuta hisia na
kumbukumbu ya mapito yake
SOMA HADITHI >>>>>>>
Post a Comment