MICHEZO/SPORTS: UCHAMBUZI WA SHAFFIH DAUDA JUU YA MECHI YA JANA>>>...
https://menacotz.blogspot.com/2012/10/michezosports-uchambuzi-wa-shaffih.html
.Wachezaji walishindwa kutambua umuhimu wa mchezo huo
. Mwamuzi alikuwa zaidi ya ‘kituko’
.Kwa nini Haruna Moshi na Mwasika walimaliza mchezo?
Mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000 timu za soka za Yanga na Simba zilicheza soka la ‘aibu’ uku wakionekana kama vile wanacheza mchezo wa ‘rugby’.
Baada ya penati iliyopigwa na mshambuliaji Said Bahanuzi kuipatia Yanga bao la kusawazisha mwishoni mwa kipindi cha pili, kiujumla timu hizo ambazo zinachukuliwa kama kioo cha soka la bongo hazikuonesha soka lolote zaidi ya kucheza kibabe na kukamiana tu.
Upande wa pili mwamuzi alishindwa kuyatolea adhabu sahihi baadhi ya matukio makubwa kwenye mchezo huo, Haruna Moshi aliyeingia dakika 20 za mwisho alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu, alimrukia kwa makusudi beki wa Yanga, Kelvin Yondan na ni dhahiri alitaka kumvunja. Ni aibu ambayo dunia imeishuhudia, lakini tumepata fursa nzuri ya kutangaza ‘msisimko’ uliopo katika mpira wetu kutoka kwa mashabiki.
Post a Comment