SITAISAHAU facebook
https://menacotz.blogspot.com/2012/11/sitaisahau-facebook_28.html
MTUNZI: Emmy John P.
CONTACTS: 0654 960040
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA
ILIPOISHIA
John alipogeuka ile alama ya kuchanwa na kisu ikaonekana. Nikabaki kama zoba siwezi kupiga kelele wala kutoa msaada wowote.
John alipogeuka ile alama ya kuchanwa na kisu ikaonekana. Nikabaki kama zoba siwezi kupiga kelele wala kutoa msaada wowote.
Huyu naye akageuzwa shingo, kisha ghafla pakawa giza sikuweza kuona mbele. Lakini nilihisi kama napoteza fahamu hivi.
Huyu naye akageuzwa shingo, kisha ghafla pakawa giza sikuweza kuona mbele. Lakini nilihisi kama napoteza fahamu hivi.
Macho yalipopatra ujasiri na kufunguka nilikuwa nimezungukwa na watu wenye nguo nyeupe.
Macho yalipopatra ujasiri na kufunguka nilikuwa nimezungukwa na watu wenye nguo nyeupe.
Kila jicho likinitazama mimi.
Kila jicho likinitazama mimi.
Hofu mpya ikaanza.
Hofu mpya ikaanza.
***ISABELA katika mtihani mwingine!!!!
***ISABELA katika mtihani mwingine!!!!
ENDELEA
******
Watu hawa walitabasamu vizuri lakini sikujua kwa nini wanatabasamu.
“Pole sana!!.” Mmoja wao aliniambia.
“Nini kwani…eeh!! Hapa ni wapi.”
“Hospitali ulipoteza fahamu.” Mwanaume aliniambia.
Sasa akili ilianza kuunganika upya nikawatambua kuwa wale ni madaktari.
Kilichonisibu nikashindwa kukielewa vyema. Nikavuta kumbukumbuku
nikakumbuka kuwa ni ndoto. Ndoto nyingine ya maajabu. Ndoto iliyonifanya
nizimie dah!! Hii ilikuwa hatari zaidi ya kawaida.
Nikatamani kumshirikisha mtu yeyote kati ya wale madaktari lakini nikaamini kuwa hawataelewa.
Mtu sahihi wa kumueleza ni John. Huu ni wakati muafaka wa kumueleza
kila kitu kinachotokea. Ni John pekee ambaye anaweza kunielewa juu ya
shida hii. Sikuona mtu mwingine wa kumueleza.
Nilipumzika kwa masaa
kadhaa kisha John akaruhusiwa kuondoka na mimi. Ni yeye aliyenileta pale
hospitali baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimezimia.
Ilikuwa ni
tukio la kawaida mtu kuzimia lakini lilikuwa si la kawaida kwa sababu
aliyezimia ni Isabela. Mtu mwenye heshima zake pale chuoni. Kila mtu
alitaka kujua nini kimenisibu. Nashukuru John alikuwa akiwajibu kwa
niaba yangu.
Sasa tulikuwa chumbani. John alinikorogea uji wa ulezi
akatia maziwa na pilipili manga. Alijua kuwa ninaupenda sana uji wa aina
hiyo.
Nilipomaliza kunywa kikombe cha kwanza. Nilitaka kuanzisha ile mada juu ya nini kilinitokea ndotoni.
Maajabu!! Nilipomuita naye aliniita ndani ya sekunde hiyo hiyo. Tukajikuta tunacheka.
“Nani sasa aitike ya mwenzake.”
“Ladies first.” John alidakia. Basi sikuwa na ujanja mimi nikaitika nimsikilize John anasema nini.
“CR (Class representative) wa PR (Public relation)….”
“Amekufa??.” Niliuliza hata kabla John hajamaliza kunieleza. Tayari picha ilianza kuja kichwani.
“Yeah! Umejuaje kwani?.” Aliniuliza.
“Ni yule alikuwa ndugu yako au sio..”
“Ni yeye Michael ndio jina lake. Binamu yangu.” Alisema kwa masikitiko
makubwa sana John kisha akainama. Hapakuwa na haja ya kuuliza kama
alikuwa anajizuia kutoa machozi.
“Pole John.” Nilimwambia kwa sauti ya chinichini.
“Wamemnyonga binamu yangu wameona kumuua Jesca haitoshi aaah!!.”
Alilalamika mwisho akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa sauti ya juu.
Nikawa katika hali mbili ghafla. Kwanza hofu kubwa kwani alichozungumza
John sasa kilitaka kuwa kile ambacho nilikiota. Pili nikawa katika
kumbembeleza Michael kwa juhudi zote. Huku nafsi ikiniambia
ninambembeleza muuaji.
Lakini muuaji gani huyu sasa asiyejitambua kuwa ameua? Nilijiuliza.
Nikahisi kuchanganyikiwa.
“Isabela.” Aliniita.
“Bee!!.”
Post a Comment