BREAKING NEWZZ# MGOMBEA URAIS WA CHUO KIKUU CHA SAUT TABORA (AMUCTA) AJITOA KWENYE NAFASI HIYO

>AMWACHA MAKAMU WAKE PEKEE YAKE

>SAA CHACHE KABLA YA SCREENING YA MWISHO

>ADAI HAKUNA DEMOKRASIA YA KWELI

>MWENYEKITI WA TUME ASHITUSHWA NA UAMUZI HUO


      Katika hali ya kushangaza, mgombe Urais wa chuo kikuu kishiriki cha SAUT TABORA (AMUCTA) amejiondoa katika kinyang'anyiro hicho leo asubuhi masaa machache kabla ya uchaguzi. alipofuatwa na kuulizwa na Blog hii (MeNaco.com)  Bwana Waryoba (Spika wa bunge lililopita)alikuwa na haya ya kusema " Ujue hapa chuoni ni kazi sana na hakuna demokrasia ya kweli" hata hivyo alipotakwa kufafanua zaidi kauli yake alisema " Nilikuwa na Koboli kama mgombea mwenza wangu, laikini muda uliongezwa bila sababu za msingi na kesho yake Koboli akachukua Form ya Urais bila hata kunishirikisha, na hapo nilishindwa kuelewa ni kwanini Anikimbie na kuchukua form nyingine???" alipoulizwa kama hilo ndilo analotia shaka nalo tu, akajibu " Hapana! ila nina jambo ambalo kwa sasa siko tayari kuliweka wazi ila wewe fahamu yakuwa siwezi kufanya kazi na hali hii, nawaomba radhi wana-AMUCTA wenzangu kwani nitakuwa nimewasaliti sana." 

     Hata hivyo MeNaco.com haikuishia hapo bali ilimtafuta mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuzungumzia jambo hilo na kama tayari anazo taarifa hizo, Ndugu Godfrey Maliseli alikuwa na haya ya kusema " Kiukweli nimezipata taarifa hizo na tayari nimeshaletewa barua kutoka kwa Warioba ikieleza kuwa anajiondoa kwenye ugombea Urais" pia alipoombwa kueleza nini chanzo cha yeye kujiondoa alikuwa na haya ya kusema, " kwenye barua ile imeeleza tu yakuwa anajiondoa kwenye nafasi hiyo na bila kutaja sababu kuu"

hata hivyo ZOEZI la kuwa  Screen wale wengine watatu waliobaki liliendelea na matokeo yatatoka muda si mrefu kuanzia sasa hivi, kampeni zitaanza kesho na saa tisa jioni kutakuwa na MDAHALO wa wagombea.


Related

UCHAGUZI 844546967081068894

Post a Comment

1 comment

Unknown said...

asante kwa taarifa, duuuh tumbo joto apo.
*MAMBO YA SIASA HAYO*

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item