MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA TABORA GIRLS TAREHE 31.01.2013
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/mahafali-ya-kidato-cha-sita-tabora_31.html
Mwanasheria
wa kujitegemea Bw.Emmanuel Mwasaka akitoa cheti kwa mhitimu wa kidato
cha Sita katika mahafali ya Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana
ambapo Bw.Mwakasaka alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana Bi.Helen Makala akizungumza
katika mahafali hayo yaliyofanyika katika shule hiyo.
Baadhi ya watumishi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana wakiwa katika mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana wakiimba nyimbo ikiwa ni sehemu ya mahafali.
Mwanasheria wa kujitegemea nchini
Bw.Emmanuel Mwakasaka amewatahadharisha wahitimu wa kidato cha Sita na
suala la ndoa za utotoni kwakuwa zimekuwa zikikwamisha maendeleo ya
kutaka kujiendeleza zaidi kielimu.
Akizungumza katika mahafali ya
kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Tabora wasichana Bw.Mwakasaka
ambaye pia ni mdau wa maendeleo mkoani Tabora,alisema ipo haja kwa
wahitimu hao kuwa na mtazamo wa kuendelea zaidi na masomo kuliko
kufikiria kuolewa wakati huu wakiwa na umri mdogo jambo ambalo huenda
likawatia kwenye matatizo katika maisha yao.
Alisema maisha ya sasa yamekumbwa
na changamoto nyingi ambapo kwa sehemu kubwa ya maisha yanahitaji
kujitosheleza zaidi kielimu ili kuweza kuyamudu.
''Hivi sasa jamani mtakuwa katika
kipindi kigumu sana wakati huu mnapokwenda majumbani kwenu,changamoto ni
nyingi hasa mbaya zaidi kwa ninyi mnaokwenda vijijini,maana huko si
ajabu mnaweza kuwa wazazi au walezi wenu wamekwisha chukua fedha kwa
ajili ya kuwaozesheni"alisema Mwakasaka.
Hata hivyo Bw.Mwakasaka pamoja na
kuahidi kusaidia komyuta tatu,Projekta moja na Jenereta moja katika
Shule hiyo alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wanaobaki Shuleni hapo
kuona umuhimu wa masomo ya Sayansi ambayo kimsingi alidai kuwa yamekuwa
yakitoa ajira kwa wingi kuliko masomo mengine ulimwenguni.
Kwaupande wake mkuu wa Shule hiyo
ya Tabora Wasichana Bi.Helen Makala katika risala yake kwenye mahafali
hayo alisema kukosekana kwa uzio katika Shule hiyo ni moja ya changamoto
kubwa na ni tishio kwa maisha ya wanafunzi hao wakike.
Alisema licha ya Shule hiyo
kufanya vizuri lakini wanafunzi wamekuwa wakiishi katika mazingira ya
wasiwasi kutokana na vibaka kuvamia mara kwa mara na kuiba nyakati za
usiku.
"Shule hii ina eneo la hekta 97.4
hakuna uzio wowote hata wa kuzunguuka eneo dogo linalozunguuka
majengo,mazingira haya ni hatarishi zaidi kwa wanafunzi wa kike wakiwemo
albino na wasioona"alisema mkuu huyo.
Aidha
Shule ya Tabora wasichana ambayo ni ya bweni ilianzishwa mnamo mwaka
1928 ikitajwa kuwa baadhi ya viongozi wakubwa wanawake wa serikali ya
Tanzania wamesoma katika shule hiyo ambayo kwasasa inajumla ya wanafunzi
wapatao 610.
CHANZO: KAPIPI JHABARI.COM
Post a Comment