RAIS JAKAYA KIKWETE AUNG'URUMA KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA WANACHAMA WA MPANGO WA AFRIKA KUJITATHMINI KIUTAWALA BORA (APRM) ADDIS ABABA
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/rais-jakaya-kikwete-aunguruma-kwenye.html
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubua mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa
Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM)
baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia leo Januari
27, 2013 katika makao makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.
Mhe.
Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda
nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo
Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe. Rais
Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge
wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Jakaya
Mrisho Kikwete na ujumbwe wake akitoka nje ya ukumbi baada ya
kuhutubua mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa
Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) baada ya kuwasilisha
ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia leo Januari 27, 2013 katika makao
makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete (wa nane toka kulia, akiwa na viongozi wenzake
katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Wakuu
wa Nchi za Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa leo Januari 27, 2013
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya
pamoja na ujumbe aliofuatana nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha
Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM, Tanzania.Picha na IKULU
Post a Comment