SIMBA ANGA KWA ANGA TU




Sehemu ya kikosi cha wachezaji wa timu ya Simba wakiwa katika mazoezi ya viunog kwenye gym mjini Muscat,Oman.

MFADHILI aliyeileta Simba katika kambi ya wiki mbili mjini hapa, ameaahidi kuwa kambi za Simba kujiandaa na michuano mikubwa zitakuwa zikifanyika nje ya nchi tu, ikimaanisha kuwa wachezaji sasa watakuwa wakiruka kutoka anga mmoja na kwenda anga jingine kwa ndege.

Mfadhili huyo, Rahma Al-Kharusi ambaye ni mfanyabiashara wa mafuta alisema kuwa baada ya kuiweka Simba kwa wiki mbili nchini Oman, sasa amepanga kuipeleka katika kambi nyingine huko Qatar.

Hata hivyo aliwaweka kitimoto wachezaji wa Simba na kuwataka kuachana na tabia mbaya kama kuvuta bangi na akawataka waahidi kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza katika kikao maalumu jana Jumatatu katika hoteli ya Al- Madinah Holiday mjini hapa, Rahma alimpa namba ya simu nahodha wa Simba, Juma Kaseja ili awe anawasiliana naye iwapo wachezaji watakuwa na matatizo yoyote.

Kikao hicho kilichochukua saa nzima, kiliongozwa na Rahma Al- Kharusi, Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, Musley Al- Rawahi �Ruwehi�, Kocha Mkuu Patrick Liewig, na maofisa wengine wa benchi la ufundi; Jamhuri Kihwelu na Moses Basena.

Rahma ndiye aliyeanza kuzungumza na kuwaambia wachezaji kuwa wanatakiwa kubadilika kwa kuachana na tabia za awali huku akiwaahidi kuweka kambi nje ya nchi kila wakati na kwamba baada ya Oman inayofuata itakuwa Qatar. �Mnatakiwa mjitambue kwa sababu haya ni maisha, hakuna aliyeanza kwa kujua,�alisema Rahma, ambaye anamiliki kampuni ya RBP Group inayojihusisha na uuzaji wa mafuta.

�Tabia ambazo mlikuwa nazo awali kama mabangi na mengineyo muachane nayo na muwe na malengo ya mbali kama mnataka kufanikiwa,� alionya.
�Tena nawaambia nyie kambi yenu itakuwa ni nje ya nchi tu na mpango unaokuja ni Qatar lakini mfanye kazi kwanza.�

Alisema atakuwa upande wa wachezaji kutetea maslahi yao na ili kuwahakikishia hilo, alimpa namba yake ya simu nahodha Kaseja ili kama kuna malalamiko waeleze ili watafute njia ya kumaliza. Kocha Mkuu, Patrick Liewig alisema: �Kama mlivyosikia naomba muahidi hapa kuwa mtatimiza kila kitu tutakaporudi Dar es Salaam kujituma na hasa nidhamu. Mmepata kila njia ya kufanya sasa msiniangushe.�

Naye, Julio alisisitiza kwa kuwapa changamoto ya kufanya vizuri na kuwatolea mifano mbalimbali ya awali wakati wao walipokuwa wanacheza mpira.

Simba ipo kambini Muscat, Oman tangu Januari 9 inatarajia kutua
Dar es Salaam kesho Jumatano na ndege ya Shirika la Oman                                                                                    CHANZO: MWANASPOTI
 

Related

SIMBA SC 1211398263419955848

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item