Wafa wakigombea mjane; Auawa kwa kumwaga pombe ya mwenziye

Wanaume wawili wameuawa mmoja kwa kuchomwa visu na  mwingine kwa kupigwa na mawe, wakati wakigombea mwanamke mjane Wilayani Tarime mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Kipolisi wa Tarime na Rorya, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo lilitokea juzi eneo la gulio katika kijiji cha Nyibaso, tarafa ya Ingwe, wilayani Tarime kwa sababu ya  wivu wa mapenzi.

Alisema wanaume hao walikuwa wanagombania mwanamke ambaye mume wake alishafariki dunia.

Alisema katika tukio hilo, mmoja wao, aliyetambuliwa kwa jina moja la Nyamureba, mkazi wa kijiji cha Matanka, wilayani Serengeti, alimshambulia Juma Mseti au Marwa (20), mkazi wa kijiji cha Nyibaso, kwa kumchoma visu tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo. Baada ya kumuua mwenzake, mwanaume huyo alikimbia lakini wananchi wakiongozwa na ndugu wa marehemu, walimfukuza na kufanikiwa kumkamata na kumchoma visu na kumpiga kwa mawe hadi alipokufa papo hapo.

Alisema mwanamke aliyekuwa anagombaniwa na wanaume hao alitoroka.

Kwenye tukio jingine, Jeshi la Polisi katika mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya, linamtafuta mwanaume kwa tuhuma za kumuua mwenzake kwa kumkata panga na kumchoma kisu baada ya kumwaga pombe yake ya kienyeji.

Tukio hilo lilitokea eneo la machimbo ya dhahabu ya kienyeji yaliyoko Itandula.

Kamanda Kamugisha, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:45 jioni katika kitongoji cha Itandula, kijiji cha Nyakunguru, wilayani Tarime. Alimtaja mwanaume anayetafutwa na jeshi hilo kuwa ni Makuri Mcharo, mkazi wa kikijiji hicho na marehemu ni Makuri Hamisi (32), pia mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda Kamugisha amewataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na pia kuwasihi kupunguza ulevi kutokana na matukio ya watu kuuana wakiwa wamelewa ni mengi wilayani humo.

via NIPASHE

Related

VIFO 4135158009311353728

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item