BREAKING NEWZZZZ!!!!!: BUNGE LATOA TAMKO JUU YA UONYESHWAJI WA BUNGE LIVE AU RECORDED
https://menacotz.blogspot.com/2013/02/breaking-newzzzz-bunge-latoa-tamko-juu.html
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
__________
TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI
______________
BUNGE LA TANZANIA
__________
TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI
Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge. Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge. Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwakuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti. Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kunaRadio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD,BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa. Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendeleakutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazokwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazoyatakayotolewa na mitandao ya Bunge. Utaratibu huu unatokana na uamzi wapamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bungevitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwajuu ya mawasiliano TCRA. Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahirikwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio auTecknohama, bali linatarajia kuboreshaupatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pandezote, yaani Bunge na Wananchi. Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayokwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupatafeedtoka katika mitambo ya Bunge, napale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursahiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajirihiyo. Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati. Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe. Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan). Hivyo basi, wakati zoezi la maboreshohayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwambatunaendelea kusisitiza tena, Wananchiwasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitishamatangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima lamaboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge. Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.
Dr. Thomas D.Kashililah
KATIBUWA BUNGE
KATIBUWA BUNGE
Post a Comment