YANGA HOI KWA MTIBWA>>>> ZATOKA SARE 1-1
https://menacotz.blogspot.com/2013/02/yanga-hoi-kwa-mtibwa-zatoka-sare-1-1.html
Vinara wa
Ligi kuu soka Tanzania Bara ambao pia ni Mabingwa wa Kombe la KAGAME Yanga SC
leo jumamosi Feb 02,2013 imepunguzwa
kasi baada ya kulazimishwa sare ya
kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Hadi
mapumziko, Mtibwa walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na kiungo wa
zamani wa Simba SC, Shaaban Kisiga dakika
ya 44 ya mchezo huo.
Kisiga
aliyewika pia SC Villa ya Uganda na Azam FC ya Dar es Salaam alifunga bao hilo
akiunganisha kwa kichwa kona maridadi ya beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
Kipindi cha
pili, Kipa Hussein Sharrif ‘Cassillas’ alizuia michomo mingi ya washambuliaji
wa Yanga ambao walikua wakihaha kusaka mabao, lakini Mtibwa walikuwa imara hii.
Aidha mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza
‘Diego’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Didier Kabumbangu
aliyeinusuru Yanga kuzama katika mchezo huo wa leo baada ya kufunga bao la
kusawazisha dakika ya 86, akiunganisha pasi nzuri ya Said Bahanuzi aliyetokea
benchi pia kuchukua nafasi ya Frank Domayo.
Ligi hiyo
soka Vodacom Tanzania bara itaendelea hapo kesho Februari 03.02.2013. kwa Mabingwa watetezi wa kombe
hilo Simba SC v JKT Ruvu [UWANJA WA
TAIFA, DSM] ili hali Coastal Union v Tanzania Prisons [MKWAKWANI, TANGA]
Matokeo hayo
yanaifanya Yanga itimize pointi 33 baada ya kucheza mechi 14 na inaendelea
kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 32, zote zimecheza mechi 14.
Post a Comment