TABORA MARATHON 2013 YAFANA
Tabora Marathon 2013, ilishirikisha
mbio za
Nusu Marathon Kilomita 21 kwa
wanaume,
Kilomita 15 kwa wanawake na
Kilomita 5
kwa watoto na wazima.
Katika kilomita 21, mshindi wa
kwanza
aliibuka Tabu Mwandu aliyetumia
saa
1:10.35 aliyezawadiwa kitita cha sh
100,000, kikombe na medali ya
dhahabu,
wa pili Dickson Mkami saa 1:13.18
na
kujipatia sh 70,000 medali ya fedha
huku
nafasi ya tatu ikienda kwa Francis
Jombe
aliyetumia saa 1:14.36 na
kuzawadiwa sh
60,000 na medali ya shaba.
Aidha kilomita 15 wanawake, Grace
Jackson alishinda akitumia dakika
55:33.06
na kuzawadiwa sh 100,000, medali
ya
dhahabu na kikombe, wa pili
Maombi
Elisha dakika 58:52.01 na
kuzawadiwa sh
70,000 na medali ya fedha huku
nafasi ya
tatu ikienda kwa Naomi Samweli
aliyetumia saa 1:00.05 aliyejipoza
kwa sh
60,000 na medaliya shaba.
Kwa kilomita 5 wanaume wa
kwanza
aliibuka Robert Mayala wa pili ni
Joseph
Kimatile na kufuatiwa na Rashid
Malugu
waliopata medali za dhahabu,
fedha na
shaba.
Upande wa wanawake kilomita tano
ni
Getruda Musa wa pili Sara Lyimo
na Asha
Seleman ambao nao walipata
medali, huku
mkimbiaji mwenye umri mkubwa
Msese
Said (65), Msese Said akipata fedha
sh
17,000 kutoka kwa akiwamo DC
Kumchaya.
HABARI: NASSOR WAZZAMBI
Post a Comment