WEMA, DIAMOND ‘WAVUANA NGUO’


Wema Isaac Sepetu.
Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Na Sifael Paul
NI mwendo wa ‘kuvuana nguo’ hadharani, kuchambana na kupakana matope hadharani kwa mastaa wawili wa Kibongo ambao ni wapenzi zilipendwa, Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Kufuatia Wema kudhalilishwa na Diamond kwa kukataa kupokea fedha alizotaka kumtunza alipokuwa ‘akipafomu’ kwenye shoo yake ya Diamonds Are Forever katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, kwa sasa mmoja akisema hili, mwenzake anaibuka na kusema lile, lengo likiwa ni kuharibiana.
HUYU HAPA WEMA
Kwa mujibu wa Wema, kitendo cha Diamond kukataa kupokea fedha zake ni ushamba huku akisisitiza kuwa ni uswahili na hakutegemea angemfanyia hivyo kwa sababu yeye ni shabiki wake kama walivyo wengine.
NI USHAMBA
“Ule ni ushamba, alichofanya nasisitiza ni uswahili, lakini mimi nitazidi kuwa shabiki wake na ‘kumsapoti’.
“Ukweli ‘alinidisapointi’ sana, sikujua ni mshamba kiasi hiki, anatakiwa ajue yeye ni msanii mkubwa ‘so’ hakupaswa kuwa na mambo ya ajabu.
“Unajua hata kama tumeachana, sisi siyo maadui, kuna leo na kesho,” alisema Wema alipotinga ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, Dar, Jumatatu wiki hii.

ETI WEMA ANATAFUTA UMAARUFU KUPITIA DIAMOND!
Makubwa! Kwa upande wake Diamond alimjibu mrembo huyo kuwa aache kutafuta umaarufu kupitia jina lake huku akimtahadharisha kuwa anataka kumharibia uchumba wake kwa anayempenda (hakumtaja).
“Wema anatafuta umaarufu kupitia kwangu, anataka kuniharibia kwa mchumba wangu na aache kunifuatilia,” alisema Diamond, kauli ambayo ilimkera Wema na kumjibu hewani alipokuwa akihojiwa na Radio Clouds FM:

WEMA MSHTUKO
“Mimi? Natafuta umaarufu kupitia jina lake? Ha! Mimi nimekuwa staa tangu 2006 (aliposhinda Taji la Miss Tanzania), Diamond alianza kujulikana 2010 jamani! Please! Diamond ‘amenidisapointi’ sana, ajirekebishe.”

BADO WANAPENDANA?
Kwa mujibu wa wadau waliofuatilia ‘sheshe’ la wawili hao ambalo limekuwa gumzo Bongo, Wema na Diamond wana ‘elementi’ za mapenzi ndani yao hivyo kinachotokea ni wivu ambao kila mmoja anao kwa mwenzake.
Mastaa hao walimwagana hivi karibuni huku kila mmoja akidai mwenzake ni tatizo na tangu wameachana imekuwa ikielezwa kuwa bado wana mawasiliano ya ukaribu.

source: Global publishers Limited

Related

Celebrities 8670432775569947625

Post a Comment

1 comment

Anonymous said...

mafala

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item