MUENDELEZO WA HABARI PICHA JUU YA KIFO CHA KANUMBA

MAREHEMU STEVEN KANUMBA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KWA HESHIMA KUBWA, KWELI ALIKUWA MTU WA WATU

  MeNaco.comkutoka mjini Tabora  inakumuvuzishia matukio ya mwisho ya mazishi ya Marehemu Steven Kanumba kupitia sitelite zake zilizokuwa zikimalizia kazi hiyo kwenye makaburi ya Kinondoni baada ya kutoka pale Leaders,kama inavyoonyesha kwenye picha hii ya kwanza.  
Waombolezaji wa msiba wa Marehemu Steven Charles Kanumba wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu  kwenye kaburi, tayari kwa kumpumuzisha katika nyumba  ya milele kwenye makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo  jioni  , Kanumba atakumbukwa kwa kazi yake nzuri katika tasnia ya filamu hapa nchini, ambapo alijitangaza na kuitangaza nchi vyema ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania kupitia filamu zake nyingi alizoigiza.
(MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN)
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiuaga mwili wa mwanaye kwa mara ya mwisho kabla ya kuzikwa rasmi katika makaburi ya Kinondoni.
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa na ndugu wa karibu wakiaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho makaburini Kinondoni.
 Waombolezaji wakitayarisha jeneza la marehemu Steven Kanumba tayari kwa kuliweka kaburini.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa baada ya kupoteza fahamu makaburini.
 Wajenzi wa kaburi la marehemu wakichanganya Sementi kwa ajili ya kufukia.
 Maqma wa Marehemu Steven Kanumba akiweka shada la maua mkaburini
 Wafanyakazi wa msalaba mwekundu wamefanya kazi ya ziada kutoa huduma ya kwanza kwa waombolezaji
 Maskari wa kusimamia usalama wakiweka uzio kwa ajili ya kuhakikiosha usalama katika mazishi hayo.
 Polisi wakiweka ulizi wa kutosha katika mazishi hayo.
 Kamanda wa Kanda Maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waombolezaji makaburini Kinondoni.
 Umati huu wote uko makaburini na wengine kama unavyoona wamepanda kwenye miti ili mradi tu waone mazishi ya mpendwa wao Steven Kanumba.
Mwanamitindo maarufu mtanzania anayefanya kazi zake za mitindo nchini Marekani Millen Magese akienda kuweka shada la Maua kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba.

YALIYOJIRI KATIKA VIWANJA VYA LEADERS WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA LEO

 Fullshangweblog.com inakuletea matukio kadhaa yaliyojiri katika viwanja vya Leaders wakati wa tukio kubwa la kuuaga mwili wa Mwigizaji marehemu Steven Kanumba kama picha hii ya kwanza inavyoonyesha Makamu wa Rais akimfariji mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa, wakati alipokwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu mwigizaji huyo aliyefanya vizuri sana katika tasnia ya filamu nchini Tanzania na nje ya Tanzania.
 Waigizaji mbalimbali wakiwa katika msiba huo kwenye viwanja vya Leaders leo.
 Rais wa shirikisho la filamu Nchini Bw. Saimon Mwakifwamba akimfariji mmoja wa waombolezaji katika msiba huo.
 Mmoja wa waombolezaji akibebwa juu juu baada ya kuzirai katikamsiba huo.
 Huyu naye hakujiweza ilibidi asaidiwe na wafanyakazi wa Msalaba mwekundu.
 Huyu muombolezaji naye alidondoka baada ya kupoteza fahamu na kuzirai katika viwanja vya Leaders.
 Watoto waliowahi kuigiza na marehemu Steven Kanumba na ambao aliibua vipaji vyao yeye mwenyewe wakiwa wamebea picha ya Marehemu Kanumba.
 Hali ilikuwa ni ya majonzi na waombolezaji wengi walidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na simanzi.
 Viongozi mbalimbali wamehudhuria katika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe, Waziri wa Ardhi na Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Idd Azzan.
Mtangazaji wa Clods TV Regina Mwalekwa akiwajibika katika tukio hilo la kihistoria kwenye viwanja vya Leaders


CHANZO: FULL SHANGWE

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item