https://menacotz.blogspot.com/2011/07/chuo-kikuu-cha-dar-es-salaam-udsm.html
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametishia kuanzisha mgomo hivi karibuni, endapo Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) haitawapatia fedha za mafunzo ya vitendo kabla ya kuanza kwa mitihani ya kufunga chuo Julai 11, mwaka huu.
Mjadala huo wa kutaka kugoma ulianza katika mkutano wa Bunge la Serikali ya Wanafunzi (Daruso), uliokuwa ukijadili bajeti ya chuo hicho na badala yake kuahirishwa baada ya kuonekana kuwepo taarifa ya mabadiliko katika utoaji wa mikopo.
Spika wa Bunge hilo, Peter Anord, alisema Waziri wa Bodi ya Mikopo alitoa taarifa ya kutolewa kwa fedha hizo jana, lakini baada ya wanafunzi kufuatilia katika ofisi za HELSB walipewa taarifa ya fedha hizo kutolewa baada ya mitihani kumalizika.
“Taarfa iliyotoka kwa mkuu wa mikopo inasema fedha hizo zitatoka baada ya mitihani kumalizika ambapo ni kinyume cha sheria na taratibu za chuo kwani hapo awali tulikuwa tanapewa kabla ya kuanza kwa mitihani,” alisema Anord.
Pia, alisema juzi yalitolewa majina ya wanafunzi ambao watapatiwa fedha hizo baada ya mitihani kumalizika Juni 25 huku wengine zaidi ya 500 wakiwa hawaoni majina yao, jambo ambalo wanafunzi hao wanaona kama ni usumbufu.
“Majina yametolewa, lakini pia fedha ambazo zitatolewa ni kwa madaraja tofauti tofauti ukilinganisha na mwanzo walikuwa wanatoa kwa usawa, na pia wamefanya mabadiliko kwa wanaoenda mikoani kwa kuwapatia fedha ya nauli ya kwenda tu bila ya kurudia na kuzigawa nauli hizo kwa asilimia 10 kwa madai ya kuepuka udanganyifu wa wanafunzi ambao hawafanyi mafunzo hayo nje ya Mkoa,” alisema Anord.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment