FIFAYARUHUSU ITC YA KAGO ITOLEWE
https://menacotz.blogspot.com/2011/08/fifayaruhusu-itc-ya-kago-itolewe.html
20
Aug
FIFA imeruhusu ITC itolewe baada ya kubaini kuwa Simba ilituma maombi ya kuomba hati hiyo ndani ya muda uliopangwa, lakini CAR ilishindwa kufanyia kazi. Hivyo kinachosubiriwa sasa ni CAR kutuma ITC hiyo.
Licha ya FIFA kuagiza hivyo, TFF imeitaka Simba kukata jina moja kati ya sita ya wachezaji wa kigeni ilionao katika orodha yake. Kanuni ya Ligi Kuu ya Vodacom inaruhusu timu kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.
Wachezaji wa kigeni ambao Simba ina mikataba yao ni Derrick Walulya, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu, Gervais Kago, Patrick Mafisango na Jerry Santo.
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji wakati ikipitia usajili iliagiza kuwa Walulya ambaye Simba ilisema imemuacha ni mchezaji wake kwa vile bado ina mkataba nayo. Hivyo inachotakiwa kufanya Simba ni kuvunja mkataba wa mchezaji mmoja ili kubaki na watano
Post a Comment