Ferguson miaka 25 Man Utd, mechi 1,409



LONDON, England
KOCHA Alex Ferguson kesho Jumapili anatarajia kutimiza miaka 25 akiifundisha klabu ya Manchester United.
Akiwa ametwaa mataji 27, anaelezwa kuwa ndiye kocha mwenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la England.
Ferguson, 69, anasifika kwa kuwekeza mbinu nzuri za ufundishaji kwenye dimba la Old Trafford kufikia mafanikio hayo, huku pia akielezwa kama 'kocha mwenye akili sana'.
Akiwa na rekodi ya kuwa kocha aliyekaa muda mrefu katika historia ya makocha wa Man United, Ferguson ataiongoza United kucheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Sunderland kesho siku yake ya kutimiza miaka 25, ikiwa ni mechi yake ya 1,409 tangu alipojiunga mwaka 1986.
Ferguson aliwasili Old Trafford Novemba 1986 akiwa na malengo ya kuvunja utawala wa soka la England uliokuwa mikononi mwa Liverpool.Jukumu hilo alifanikiwa kulitekeleza na baada ya kipindi chote hicho, Liverpool imefunikwa kabisa na maendeleo ya United.
Ilikuwa kazi kubwa, kwani Liverpool ilikuwa timu ya kwanza kutwaa mataji matatu kwa mpigo tangu mwaka 1971, na mara 16 ubingwa wa England dhidi ya mara saba kwa United.
Lakini kocha huyo wa Scotland, ameacha historia kwa kutwaa mataji 12 ya ubingwa wa England, makombe mawili ya Ligi ya Mabingwa, mataji matano ya Kombe la FA na Kombe la Dunia la FIFA kwa vilabu.
Taji la mwaka jana la Ligi Kuu ya England, limeifanya United kufikisha 19 na kuizidi Liverpool yenye mataji 18.
"Ni kocha mwenye akili sana," alisema Charlton. "Kuna makocha wengi vijana kwenye mchezo wa soka kwa sasa. Lakini yeye ni wa muda mrefu, alizaliwa kwa ajili ya soka. Ni kocha mwenye kipaji."
"Ni ngumu zaidi kufananisha kipaji na uwezo wa Alex kocha na mwingine kwa sasa.
"Amekuza vipaji vya wachezaji kama David Beckham, Ryan Giggs, Eric Cantona, Bryan Robson, Wayne Rooney, Ruud van Nistelrooy na Cristiano Ronaldo.Labda kocha Jos Mourinho wa Real Madrid anaweza kuwa mfano, hata hivyo hajawahi kukaa na klabu moja kwa zaidi ya miezi 35."
Wakati kocha Mourinho haoni taabu kuondoka sehemu ambayo anaona hakuna raha, kwa Ferguson ni tofauti kwani amekuwa mvumilivu na asiyependa sana malumbano.

Ni mara moja Ferguson, aliwahi kusema kwamba anafikiria kustaafu kufundisha katika misimu wa mwaka 2001/02.
Hata hivyo, alibadilisha mpango huo wa kujiuzulu ambapo tayari United ilijiandaa kumuazima kwa muda aliyekuwa kocha wa England wakati huo Sven-Goran Erikkson kama hasingebadili maamuzi yake.
Ferguson amekutana na mabadiliko mengi katika mchezo wa soka tangu alipojiunga na United kwa mara ya kwanza Novemba 6, 1986.
Wakati akianza kuifundisha United, hakukuwa na mashindano ya Ligi ya Mabingwa wala Ligi Kuu, na wakati huo makipa walikuwa wakiruhusiwa kudaka mpira unaorejeshwa kwao.
Katika historia ya soka la England, hakuna kocha aliyekaa madarakani kiasi hicho na kupitia mabadiliko hayo na mengine mengi.

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item