MSANII CHIPUKIZI DYANKA G WA BONGO FLAVA AFUNGUKA MENGI DHIDI YA USANII, KAZI, NA MATARAJIO YAKE
https://menacotz.blogspot.com/2012/06/msanii-chipukizi-dyanka-g-wa-bongo.html
DYANKA G (ZAMANI G-SOJA)
SIKILIZA NGOMA ZAKE HAPO JUU
HAMASA YA KUIMBA ALIKUWANAYO TANGU MDOGO LAKINI ILIPOFIKA MNAMO MWAKA
2002 HATAMU ILIFIKIA UPEO MKUBWA, 2006 NDIPO NDOTO ZAKE ZIKAMWAGIKA PALE
ALIPOFANIKISHA KUFANYA NGOMA YA KWANZA ILIYOFAHAMIKA KAMA "SOJA" MWAKA
ULIOFUATA (2007) UKAWA NI WAMAFANIKIO AMBAYO KWA KIASI CHAKE
ALIFANIKIWA KUFANYA BAADHI YA SHOO NA AKINA MWANA FA, O-TEN CHINI YA
UDHAMINI MKUBWA WA TCRS (TANZANIA CHRISTIAN REFUGES' SERVICES.
ALIAMUA KUSIMAMISHA KWA MUDA ILI KURUHUSU TAALUMA IONGEZEKE KICHWANI
HADI KUFIKIA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA SAUT (AMUCTA) KILICHOPO MKOANI
TABORA.
- NIIGE MIMI
- JALALA
- FROM ZERO TO ZERO
NGOMA ZILIZOGONGWA NA PRODYUZA
MKALI G-KIFAA WA TABORA KATIKA STUDIO ZA HITIMISHO RECORDS AMBAYE KWA
SASA ANATARAJIA KUFANYA PROJECT NA TMK HALISI KAMA PRODYUZA WA KUNDI
HILO.
NGOMA ZA DYANKA G NI NGOMA AMBAZO ZIMEFANIKIWA KUFANYA VIZURI NA
KUTIKISA KATIKA TATU BORA ZA CG FM ILIYOPO TABORA, PIA ZINAVUMA KATIKA
VITUO MBALIMBALI VYA REDIO KAMA TBC FM, RK FM, MLIMANI REDIO, ISANGANILO
FM REDIO INAYOBAMBA HUKO BURUNDI.
MATARAJIO YA KUGONGA NGOMA MPYA YAMESHIKA KASI BAADA YA PRODYUZA
G-KIFAA KUMTUPIA BEAT FREE AIFANYIE MAZOEZI NA IKIWEZEKANA KUINGIA
DSM KUFANYA NGOMA HIYO AMBAYO JINA LIMEHIFADHIWA,
PIA MAMBO YANAWEZA KUNOGA ZAIDI
ATAKAPOICHAGUA MOJA YA NYIMBO ALIZOZIIMBA NAKUZIFANYIA VIDEO DSM HIVI
KARIBUNI. ANATARAJIA KUPIGA SHOO KIBONDO KIGOMA TAREHE 8/7/2012.
DYANKA G AMEFUNGUKA KUWA KUWEPO KWA MITAZAMO POTOFU DHIDI YA KAZI ZA
USANII KUONEKANA NI UHUNI KWA BAADHI YA WATU NA KUFUNGUKA KUWA MZIKI NI
KAZI KAMA KAZI NYINGINE HIVYO HAIPASWI KUDHARAULIWA WASANII. PIA ANASEMA
CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO NI KAJITABIA KWA BAADHI YA WASANII
KUONEANA WIVU NA KUBANIANA RIZIKI KWANI HUKO NI KURUDISHANA NYUMA.
KUPITIA NDOTO KALI ALIZONAZO KATIKA GAME LA MZIKI AMESEMA ANAHITAJI
MSAADA WA WATU WA KUMPA SAPOTI ILI KUFANYA YALE ALIYOYAPANIA KWANI UWEZO
ALIONAO USIJE GUBIKWA NA KUTOWEZESHWA IKIWA UWEZO ALIONAO NI MZURI.
SHUKRANI ZAKE ZA DHATI ALIZITUPIA KWA MWENYEZI MUNGU IKIWA NDIYE
ANAYEMFANYA DYANKA G KUISHUKURU KWA NGUVU SANA FAMILIA YAKE KWA SAPOTI
WANAYOMPA. PIA HAKUSITA KUMFUNGUKIA PRODYUZA WAKE WA UKWELI G-KIFAA PIA
AMINIA DJZ WA CG FM WAKIWEMO MARK ZUBBE, DJ MUBA, NA CHARLES MBADE, PIA
WADAU WA STATION YA REDIO KWIZERA FM YA NGARA AKINA BOAZY ZOBANYA, PIA
BILA KUMSAHAU DIJARO ARUNGU NA WASHIKAJI ZAKE WOTE WANAOMPA NGUVU NA
KUKUBALIKA KWA KAZI ZAKE HASA WANAPOTUMIA MUDA NA KUZISIKILIZA NGOMA
ZAKE (BIG UP WADAU)
mtafute #0756-736693/ 0714-012359
SOURCE: ALOY SON BLOG
Post a Comment