MUZIKI NA FACEBOOK YA SABABISHA KIFO

>>>>KIJANA JACKSON THOBIAS A.K.A KUSH AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI.

Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani.
Jamani tuwe waangalifu tunapotembea barabarani/relini  huku tukichati au kusikiliza muziki kwenye simu au Iphone zetu hususani tunapokuwa na earphone

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item