TFF YATANGAZA 16 BORA COPA-COCA COLA


                                                                     Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, leo limetoa Taarifa kuhusu michuano ya Copa Coca Cola na kutaja Timu 14 kati ya 16 zilizofuzu kuingia Raundi ijayo na pia kutangaza Majina ya Waamuzi 15 watakaochezesha michuano ya Kagame Cupitakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28.

 Shirikisho la Soka Tanzania, TFF,                                                 
 COPA COCA COLA:
  TIMU ZILIZOFUZU:
                                        KUNDI A=Ruvuma, Kigoma, Rukwa, Arusha
                                        KUNDI B=Tanga, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza
                                        KUNDI C=Mara, Dodoma, Kinondoni, Temeke
TFF_LOGOKUNDI D=Kilimanjaro, Kagera, Nafasi mbili zilizobaki zitaamuliwa baada ya Mechi ya leo kati ya Kusini Unguja na Tabora na wanaogombea nafasi hizo ni Pwani yenye Pointi 7, Singida (7), Tabora (6) na Kusini Unguja yenye pointi nne.
Raundi inayokuja itaanza Jumamosi Julai 7.
TAARIFA KAMILI:
Release No. 108

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 5, 2012
14 ZATINGA 16 BORA COPA COCA-COLA 2012
Wakati 16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inaanza Jumamosi (Julai 7 mwaka huu) timu 14 zitakazocheza hatua hiyo zimeshajulikana baada ya mechi zilizochezwa leo (Julai 5 mwaka huu) katika viwanja vinne tofauti.
Tanga iliyoigaragaza Kaskazini Pemba mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam imechukua moja kati ya nafasi nne kutoka kundi B. Mabao ya Tanga yalifungwa na Mbwana Musa dakika ya 30, 55 (penalti) na 58 wakati lingine lilifungwa dakika ya 53 na Issa Mwanga.
Kwa ushindi huo, Tanga iliyofikisha pointi tisa inaungana na Mjini Magharibi yenye pointi 13, Morogoro pointi 12 na Mwanza pointi 11 kutoka kundi hilo kucheza hatua ya 16 bora.
Mara iliyoichapa Mtwara mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam na kufikisha pointi tisa nayo imepata tiketi ya 16 bora kutoka kundi C ikiungana na Dodoma yenye pointi 12, Kinondoni pointi 11 na Temeke pointi tisa.
Mabao ya Mara ambayo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika ilikuwa mbele kwa 3-0 yalifungwa na George William dakika ya pili, Edson Mwara dakika ya 17 na 45, na Hassan Ally dakika ya 88. Mtwara walipangusa machozi dakika ya 36 kwa bao la Ramadhan Njunja.
Ndoto za Ilala kucheza 16 bora zimeyeyuka baada ya kulala mabao 2-1 mbele ya vinara wa kundi A Ruvuma kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Mbali ya Ruvuma iliyofikisha pointi 16, timu nyingine zilizopata tiketi ya 16 bora kutoka kundi hilo ni mabingwa watetezi Kigoma wenye pointi 12, Rukwa pointi kumi na Arusha pointi nane.


Mchuano wa kupata timu mbili za mwisho kucheza 16 bora uko katika kundi D ambalo linasubiri matokeo ya mechi ya leo jioni kati ya Kusini Unguja na Tabora itakayochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Kagera ambayo leo imeifunga Shinyanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyumbu ni moja kati ya mbili ambazo zimeingia 16 bora kutoka kundi hilo. Nyingine ni Kilimanjaro iliyoongoza kwa kufikisha pointi 18 ikifuatiwa na Kagera yenye pointi tisa.
Nafasi mbili zilizobaki zinawaniwa na Pwani yenye pointi saba, Singida (7), Tabora (6) na Kusini Unguja yenye pointi nne.
15 WATEULIWA KUCHEZESHA KOMBE LA KAGAME
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.
Waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa CECAFA.
Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item