Release No. 106
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 3, 2012
TIMU 10 TANZANIA KUCHEZA ROLLINGSTONE BURUNDI
Timu
10 za Tanzania Bara zitashiriki kwenye michuano ya Rollingstone kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 20 ambayo mwaka huu itafanyika Makamba
nchini Burundi kuanzia Julai 7 mwaka huu.
Jumla
ya timu 24 zinashiriki mashindano hayo na zimepangwa katika makundi
sita tofauti. Timu nyingine zinatoka Burundi, Kenya, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda na Zanzibar.
Timu
za Tanzania zilizoingia katika mashindano hayo ni Azam, Bishop High
School, Chakyi Academy, Coastal Union, Rollingstone, Ruvu Shooting,
Simba, TAYFA Academy, Yanga na Young Life.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa Rollingstone, Issa Karata timu zote zinatakiwa
kwenda vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji wake ili kuthibitisha umri wao.
Kamati ya Mashindano itakuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu umri wa
mchezaji yeyote.
Kila
timu inatakiwa kuwa na wachezaji 20 na viongozi watano ambao
watagharamiwa na waandaaji kwa huduma za malazi na chakula kwa muda wote
wa mashindano hayo yaliyoanzishwa miaka 13 iliyopita.
WAKENYA KUICHEZESHA NGORONGORO HEROES NYUMBANI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Kenya kuchezesha mechi ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Nigeria.
Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam atakuwa Moses Ojwang Osano.
Waamuzi wasaidizi watakuwa Peter Keireini na Elias Kuloba Wamalwa wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Thomas Onyango. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Charles Masembe kutoka Uganda.
Pia CAF imemteua Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi ya michuano hiyo kati ya Misri na Kenya itakayochezwa jijini Cairo kati ya Julai 27, 28 na 29 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment