https://menacotz.blogspot.com/2012/07/tff-yatangaza-16-bora-copa-coca-cola.html?m=0
Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, leo limetoa Taarifa kuhusu michuano ya Copa Coca Cola na kutaja Timu 14 kati ya 16 zilizofuzu kuingia Raundi ijayo na pia kutangaza Majina ya Waamuzi 15 watakaochezesha michuano ya Kagame Cupitakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28.
Shirikisho la Soka Tanzania, TFF,
COPA COCA COLA:
TIMU ZILIZOFUZU:
KUNDI A=Ruvuma, Kigoma, Rukwa, Arusha
KUNDI B=Tanga, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza
KUNDI C=Mara, Dodoma, Kinondoni, Temeke
Raundi inayokuja itaanza Jumamosi Julai 7.
TAARIFA KAMILI:
Release No. 108
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 5, 2012
14 ZATINGA 16 BORA COPA COCA-COLA 2012
Wakati 16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inaanza Jumamosi (Julai 7 mwaka huu) timu 14 zitakazocheza hatua hiyo zimeshajulikana baada ya mechi zilizochezwa leo (Julai 5 mwaka huu) katika viwanja vinne tofauti.
Tanga iliyoigaragaza Kaskazini Pemba mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam imechukua moja kati ya nafasi nne kutoka kundi B. Mabao ya Tanga yalifungwa na Mbwana Musa dakika ya 30, 55 (penalti) na 58 wakati lingine lilifungwa dakika ya 53 na Issa Mwanga.
Kwa ushindi huo, Tanga iliyofikisha pointi tisa inaungana na Mjini Magharibi yenye pointi 13, Morogoro pointi 12 na Mwanza pointi 11 kutoka kundi hilo kucheza hatua ya 16 bora.
Mara iliyoichapa Mtwara mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam na kufikisha pointi tisa nayo imepata tiketi ya 16 bora kutoka kundi C ikiungana na Dodoma yenye pointi 12, Kinondoni pointi 11 na Temeke pointi tisa.
Mabao ya Mara ambayo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika ilikuwa mbele kwa 3-0 yalifungwa na George William dakika ya pili, Edson Mwara dakika ya 17 na 45, na Hassan Ally dakika ya 88. Mtwara walipangusa machozi dakika ya 36 kwa bao la Ramadhan Njunja.
Ndoto za Ilala kucheza 16 bora zimeyeyuka baada ya kulala mabao 2-1 mbele ya vinara wa kundi A Ruvuma kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Mbali ya Ruvuma iliyofikisha pointi 16, timu nyingine zilizopata tiketi ya 16 bora kutoka kundi hilo ni mabingwa watetezi Kigoma wenye pointi 12, Rukwa pointi kumi na Arusha pointi nane.
Mchuano wa kupata timu mbili za mwisho kucheza 16 bora uko katika kundi D ambalo linasubiri matokeo ya mechi ya leo jioni kati ya Kusini Unguja na Tabora itakayochezwa Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Kagera ambayo leo imeifunga Shinyanga mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyumbu ni moja kati ya mbili ambazo zimeingia 16 bora kutoka kundi hilo. Nyingine ni Kilimanjaro iliyoongoza kwa kufikisha pointi 18 ikifuatiwa na Kagera yenye pointi tisa.
Nafasi mbili zilizobaki zinawaniwa na Pwani yenye pointi saba, Singida (7), Tabora (6) na Kusini Unguja yenye pointi nne.
15 WATEULIWA KUCHEZESHA KOMBE LA KAGAME
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.
Waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa CECAFA.
Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment
Tabs
Hot in weekRecentBLOG ZINGINE
Hot in week
-
picha haihusiani na story picha nimeitoa GPL Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini dare s salaam , katika ...
-
dada anayetisha kwenye tasnia ya filamu tanzania AUNT EZEJIEL huyu ndiye msanii mwenye kutisha saaana upande wa wakiume hapa tanzani...
-
Nembo ya TFF Dar es Salaam TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZ...
-
SN ADM. NO. SURNAME FIRSTNAME MIDDLE SEX O-LEVEL INDEX NAME 1 BAED 001 ABDALLAH IMANI M S0331/0090 - 2007 No Loan 2 BAED 002 ABRAHAM...
-
Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya seko...
-
MAREHEMU STEVEN KANUMBA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KWA HESHIMA KUBWA, KWELI ALIKUWA MTU WA WATU MeNaco.com kutoka mjini Tabora...
-
Mahafali ya mwaka wa tatu imefanyika ya wanachama wa International Movement For Catholic Students (IMCS) tawi la chuo kikuu kishiriki cha Mt...
-
HAPPY 5TH ANNIVERSARY TMH,SAMBAMBA NA UZINDUZI WA DUKA/OFISI & TRAINING CENTER ...
-
Leo hii kulikuwa na Ibada ya uzinduzi wa sare za kwaya ya USCF SAUT TABORA umesindikizwa na Kwaya ya TTC UKWATA hapa TABORA manispaa. Mhubir...
-
Kama una ndugu ama rafiki yako aliyemaliza Certificate, Diploma au Degree ya Ualimu basi Ingia kwenye hizi link hapa chini kuangalia Jina l...
BLOG ZINGINE
-
Saints QB competition to continue, Moore says - The Saints are taking their quarterback decision down to the wire, with coach Kellen Moore saying they want to continue the competition between Tyler Shoug...1 hour ago
-
Reds recognised at PFA Awards ceremony - The annual presentation has taken place at Manchester's Opera House.7 hours ago
-
THBUB YAANDAA MKUTANO WA WADAU KUJADILI HAKI ZA BINADAMU KATIKA BIASHARA - Farida Mangube, Morogoro. TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ya Denmark, imean...8 hours ago
-
Dira Ya Dunia - Kipindi cha habari, makala na mahojiano cha kila siku kuanzia saa kumi na mbili unusu jioni Afrika Mashariki10 hours ago
-
NEC YAWANOA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI BAGAMOYO,,DAR ES SALAAM,MKURANGA,RUFIJI,CHALINZE - Na Magrethy Katengu, Dar es salaam TUME huru ya Taifa ya uchaguzi NEC imewataka waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidi...4 weeks ago
-
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini ke...5 months ago
-
VOTE NOW: Goal Ultimate 11 powered by FIFA 22 - Who is the best defensive midfielder in the world? - We want to know who is the best defensive midfielder in the game currently3 years ago
-
Facts The Economist Got Them Wrong on Magufuli - *By Dr. Herman Louise Verhofstadt* * “A BIT like President Donald Trump, Tanzania’s president, John Magufuli, likes to fire employees on television. In No...7 years ago
-
KAIMU KATIBU IDARA YA VYUO,VYUO VIKUU AKABIDHI KADI 1500 KWA KATIBU HAMASA SENETI YA DAR - Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255...7 years ago
-
Bunge Lamkingia Kifua Zitto Kabwe......Lasema Bado ni Mbunge Halali na Spika wa Bunge ana Mamlaka Kisheria Ya Kutengua Maamuzi ya CHADEMA - Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua yoyote kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema). Kauli ya hiyo ya Bunge im...10 years ago
-
DISCUSSION ON EU-TANZANIA TRANSFER AGREEMENT WHICH ALLOWS TO TRIAL PIRATES CAPTURED BY EUROPEAN NAVAL FORCES IN TANZANIA COURTS - [image: 1] *From left is Political Officer Delegation of the European Union Tom Vens, Rear Admiral Commander Task Force 465 Jürgen zur Mühlen , and the Cha...11 years ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
JOIN US ON TWITTER
Text Widget
Millard Ayo – Official Website
- Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025 - 3/3/2025 - Magazeti
- Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo March 3, 2025 - 3/3/2025 - Magazeti
- Rais Samia awapaisha wanawake katika sekta ya madini - 3/2/2025 - Regina Baltazari
- Hospitali ya Kibong’oto kuwa taasisi ya magonjwa ambukizi - 3/2/2025 - Regina Baltazari
- Nanauka Foundation yakabidhi kadi za bima ya afya kwa wazee 204 Mtwara - 3/2/2025 - Regina Baltazari






Post a Comment