YANGA HATARINI KUSHUSHWA DARAJA - MADENI YA PAPIC ...
https://menacotz.blogspot.com/2012/09/yanga-hatarini-kushushwa-daraja-madeni.html
Tumepokea barua kutoka Kitengo cha Sheria cha Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpirawa Miguu (FIFA) likitutaka tuitaarifu Yanga kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na kocha wazamani wa klabu ya Yanga, Kostadin Papic. Katika malalamiko yake, Papic anadai kuwa hajalipwa malimbikizo ya mshahara wake yanayofikia kiasi cha Dola 12,300 za Kimarekani. Katika barua yake, kocha huyo anadai kuwa alikuwa akiwasiliana na maofisa na viongozi wa Yanga, lakini hakupata ushirikiano na hivyo kuamua kwenda FIFA. TFF ilifanya juhudi za kuwasiliana na Yanga kuhusu malalamiko hayo ili kujaribu kumzuia kocha huyo asishtaki FIFA, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.
SOMA STORI KAMILI HAPA >>>>>>>>>
Post a Comment