HATIA 9
https://menacotz.blogspot.com/2012/10/hatia-9.html
MTUNZI: George Iron Mosenya CONT: 0655 727325
“Shiit!!! Nimeacha mguu wangu ndani ya gari!!!” John alijisonya baada ya kugundua amesahau bunduki yake garini, haukuwa utaratibu wake kutembea bila silaha. Lakini hakujisumbua kusimama na kuifuata. Kauli hiyo ilizidi kumtetemesha Michael. Ina maana ndio amekuja kunifichulia maovu yangu na kuniua hapahapa!!!! Mungu wangu, lakini nilimwambia Matha kila siku kuwa ananitia matatani ona sasa!!! Aah!! Ona sasa Matha!! Aliwaza Michael kwa uchungu na kuzitupa lawama kwa Matha kabla John hajaendelea kuzungumza “Eeeh!! Umeuliza kuwa nina maana gani, ujue Michael kuna wakati unafika lazima kila ukweli uwe wazi na uamuzi ufanyike mara moja, na uamuzi mgumu ni ule unaomuumiza aliyeuamua!!!” John aliendelea Michael akawa kimya, alikuwa amekodoa macho funda la mate alilotaka kumeza ni kama lilikuwa linataka kumshinda, koromeo lilionekana kuwa dogo lakini akajilazimisha likapita. “Michael nakupenda sana lakini………” hakuweza kuendelea John muhudumu akawa amefika na vinywaji, akawafungulia , Michael akapiga mafunda mawili kulainisha koo lake, John hakupiga funda lolote bali alitia kiasi fulani kwenye glasi yake, wakati muhudumu huyu anaondoka kupisha faragha ya Michael na John, muhudumu wa kiume kutoka jikoni naye akafika kuwasikiliza. Paja la mbuzi, weka pilipili, tenganisha sahani, ndizi nne zikaushe vizuri, mwambie huyu aongeze bia. Ni baadhi ya maneno mengi waliyozungumza na hatimaye mada ikawa imesahaulika!!! John hakuendelea na maelezo. Simu aliyopigiwa na Bruno ikawa imeingilia kati. Michael akapata ahueni!!
*******
Joyce Keto alionekana kuwa kikwazo pekee kwa John Mapulu katika mipango yake ya kujipanga upya katika shughuli zake. Alitambua ni kiasi gani wasichana ni dhaifu. Hivyo kuwa mikononi mwake lilikuwa jambo salama sana.
Iwapo Joyce angetiwa mikononi mwa polisi, lazima angesema lolote analojua kuhusu Michael hali ambayo ingemuweka matatani Michael, kijana ambaye ametokea kushibana naye.
Sasa Joyce alikuwa mikononi mwake katika nyumba ya mafichoni nje kidogo ya mji wa Mwanza. Kama ilivyokuwa kwa Michael. Joyce naye alijazwa chuki na kujihisi yupo hatiani. Hasahasa baada ya kuelezwa kuwa Michael anakabiliwa na kesi ya mauaji.
“Kuonekana kwako tu pale kituoni..unatafutwa sasa ukasaidie upelelezi. Maana Michael alitoroka.” John alimwogopesha Joyce. Kisha akamalizia kwa kumueleza juu ya Michael kumkimbia.
“Kwa hiyo mlivyotoroka, amekutoroka na wewe.”
John akakubali kwa kutikisa kichwa juu na chini.
Sumu pandikizi ikapenya katika akili ya Joyce. Akawa mtumwa wa kifikra.,
Uhusiano wa kimapenzi ambao Joyce alimueleza John kati yake na Michael haswa ndio ulimfanya John asipendezwe na kitendo cha wawili hao kukutana mapema. Alihofia kusalitiwa. Hivyo alijionya kuwa muangalifu sana.
Akaamua kumuweka Joyce mbali na Michael hadi wakati stahili utakapowadia.
SOMA HAFITHI KAMILI HAPA>>>>>>>>>>>>>
Post a Comment