SITAISAHAU facebook
https://menacotz.blogspot.com/2012/10/sitaisahau-facebook_21.html
CONT: 0654960040
2
SEHEMU YA PILI
Baada ya dakika mbili nilikuwa nimemaliza kuusoma ujumbe mrefu wa Dokta Davis. Nilikuwa natetemeka, mapigo ya moyo yalikuwa katika mwendokasi wa kutisha sana. Macho yalikuwa hayafumbi bali yanaitazama simu yangu!!! Nilikuwa simuoni Dokta Davis lakini nilikuwa katika TAHARUKI!!!!!
SIKUAMINI!!!!!
*Ni kitu gani Isabella amekisoma hadi kumtisha hivyo…
**Je ni biashara gani hiyo ya mtandao.
*** Na kipi kilimsibu Isabellla baadaye!!!!
ENDELEA.
Kilichonishangaza zaidi ni faida iliyoandikwa na Dokta Davis. Sikuipinga lakini mtaji wake haukuonekana kabisa, swali likawa ni biashara gani hii isiyohitaji mtaji lakini ina faida kubwa kiasi hichi??
Nilitaka kumuuliza lakini nikakumbuka kuwa tayari aliita biashara ya mtandao.
Shida zilizokuwa zikinikabili sikutegemea kuwa naweza kumruhusu roho wa kukataa anitawale.
Mara moja nikakubaliana na Davis kuwa naweza kuifanya biashara ya mtandao. Sikutaka hata kidogo kukumbuka kuwa katika biashara huwa kuna faida na hasara.
“Lakini tunatakiwa kuonana sasa itakuwaje!!! Au hakuna mkataba?” nilimuhoji.
“Keshokutwa kama ukiwa na nafasi njoo unipokee Airport, haitakuwa mbaya kama utakuja na rafiki yako mmoja anayejua kuongea kiingereza kiasi.” Alinijibu.
Siku hiyo ikapita, lakini haikumalizika bila maajabu mengine.
Ilikuwa saa moja jioni. Sikuwa na mpango wowote wa kupata pesa, ujumbe ukaingia kwenye simu yangu.
“Nitumie namba yako ya akaunti kuna kipesa kidogo nataka nikuwekee ili mtumie kama nauli kuja uwanja wa ndege kunipokea. Nilishangazwa na meseji hiyo kutoka katika namba ambayo hakika haikuwa ya mtandao wa Afrika mashariki. Bila kuuliza nikajibu ujumbe ule lakini haukuweza kwenda, simu yangu haikuwa na salio la kutosha.
Ni kama vile upande wa pili ulitambua hilo. Simu ikaanza kuita nikapokea. Alikuwa Dokta Davis, nilimtajia namba za akaunti yangu kwa ufasaha. Ilikuwa mara ya kwanza kusikia sauti yake.
Post a Comment