CHOZI LA FUKARA
https://menacotz.blogspot.com/2012/11/chozi-la-fukara.html
Na
DEARNA MAROTER
3
Maria alikuwa na uwezo kiasi fulani “aha Karibu shostito wangu” maria alimkaribisha “asante yaani nimekumisi shost” “aha wewe si utaki kuja kunitembelea na unakaa hapahapa mjini, utadhani tumegombana” maria aliongea na kisha kwenda kumchukulia juice ya matunda “ehe nipe mastory” maria aliongea kisha kuketi kwenye kochi “nina story gani bwana zaidi ya kuja kukusalimia na unipe ela ya mboga maana leo hata sijui nita kula nini” aliongea Mercy
“Mhh!! Ahaa, hivi Mercy rafiki yangu mbona hujielewi elewi”
SASA ENDELEA
Maria aliongea kwa kejeli
“kwanini” mercy alihoji “kwahiyo yule ndo unataka kuniambia ni mume wako
mtarariwa au wakuzugia” “Maria sina utani wala!! Jordan
ndiye chaguo la moyo wangu na sidhani kama
nitamwacha” Mercy alimjibu “aha nikikumbuka zamani ulivyokuwa unang’aa na sasa
ulivyo pauka? Mhh uzuri wako wote ahaa!! Shost umepotea njia, mbona wanaume wa
kukuoa wako wengi na ulivyo tia timu tu hapa wenye pesa zao, watakao kutunza,
wanaokupenda, wenye kukuhitaji na kukutimizia mahitaji uonekane wa kung’aa
walinifuata lakini nikashindwa kuwajibu ila mmmh” maria aliongea utazani mama
wa mipasho “sikiza Maria ninachotaka ni penzi la dhati na siyo pesa” Mercy
alimjibu “umdhaniae ndiye huwa siye, mtazichuma kwa shida lakini mwisho atakuja
kukusaliti nakwambia kwa sababu ni rafiki yangu na sipendia uwe ombaomba, kwani
utakuwa ombaomba mpaka lini relax maisha ni ujana bwana shauri lako its up to you
na nisingependa uje tena eti kuniomba ela ya mboga aha hii ni mara ya mwisho
kuombaomba kama utaki kukiacha hicho kimasikini chako utajua mwenyewe mtu
ninakuonyesha njia ya maisha alafu unajishaua unajua kupenda utakufa masikini
kwa kukitegemea hicho ki Jordan” Maria
alimpatia
ushauri kisha alimpatia fedha kidogo na Mercy aliondoka kuelekea kwake.
Siku zilizidi kusogea na Mercy alikuwa ni mwenye mawazo “hata siku moja
sijawahi kwenda saluni sijui hata nitaenda lini mhuuu” aliwaza kichwani
mwake
“hali hii ngumu sana
na niyazingatia maneno ya zafiki yangu da!! Lakini moyo umezimia kwa
Jordan sijui amenipa dawa gani” aliwaza sana na ghafla simu yake
iliita na ilikuwa namba ngeni kwake. Alipokea na kumsikiliza kisha mtu
huyo
alimsihi wakutane muda wowote lakini Mercy hakumjibu. Kwa upande wa
Jordan
alizidi kutafuta na kwa bidii na siku iliyofuata alipanga aende nyumbani
kuwataarifu ndugu na mama yake kuwa anatarajia kumtambulisha wenza wake
wa
maisha ili wajiandae na kumsalimia mama yake aliye kijijini bariadi.
Jordan: “mpenzi wangu mimi kesho nitakwenda
kumsalimia mama pamoja na ndugu pamoja na jamaa pia kuwataarifu kuwa tutakwenda
wote kujitambulisha hivyo niandalie nguo pamoja na kazawadi kadogo nilichokuja
nacho kwa ajili ya kesho”
Mercy:
sawa mpenzi wangu ila usikawie kurudi kwani nitakuwa mpweke sana” alijibu kisha kuandaa baadhi ya vitu
alivyoagizwa kuandaa na usiku walikula kisha kwenda kitandani ambapo walipiga
story nyingi na walizidi kuwekeana ahadi. Usiku ulikuwa mwema na asubuhi tayari
ndege walishangilia mawiwo ya jua ndipo walisindikizana hadi kituo cha mabasi
huku wakiongea na kumpatia salamu nyingi ndipo Jordan aliweka begi chini na
kumkumbatia mercy huku akiimba
Jordan: “mpenzi ninakwenda safari, Mpenzi
ninakwenda safari penzi letu lilinde”
Mercy:
oho! usiwe na shaka mpenzi, usiwe na shaka mpenziii penzi nitalilinda”.
Walikubatiana kwa muda kisha gari lilikuwa limewasili na Jordan alipada na kupunga mkono
ishara ya kuaga kisha gari lilipotelea kwenye barabarani ya lami kwa mwendo kasi. Mercy alirudi
nyumbani akiendelaea na shughuli zake za kila siku, baada ya shughuli zake
alijipumzisha huku akionekana ni mtu mwenye mawazo mengi ndani ya kichwa chake
kwani.
Siku mbili zilipita tangu Jordan aondoke
kwenda kijjini na alikuwa amefika salama kwani mungu alimlinda katika safari
yake hiyo alifurahisana kumwona mama yake aliyeachana naye muda kwani alimpenda
sana na mama yake pia alifurahi sana, alitembeatembea kuwasalimu ndugu jamaa na
marafiki katika kijiji chao kwani alikuwa amewamiss sana. Jioni ilipofika walikuwa katika
mazungumzo na mama yake pamoja na wazee walio Karibu na familia hiyo ambao
walikuwa kama waangalizi na wazee wa kijiji
pia na ndiyo walikuwa wakitoa muafaka wa mabo waliyoshirikishwa.
SOMA HADITHI KAMILI HAPA>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Post a Comment