MTUNZI: Emmy John P.
CONT: 0654 960040
SEHEMU YA NNE
4
Nilikuwa makini katika kulikanyaga lile zulia jekundu, sikutaka kuonekana mshamba katika hilo. Nilijilazimisha kutembea mwendo wa kilimbwende wakati niliamini kuwa iwapo nitathubutu kuingia katika mashindano ya ulimbwende basi nitashika nafasi ya mwisho ama sitapata walau kigezo cha kusimama jukwaani kama mlimbwende. Maana nilikuwa cha ufupi na nilikuwa na dalili ya kuwa kibonge.
Niliongozwa hadi katika chumba kikubwa sana, kila kitu pale ndani kilikuwa cheupe kasoro ngozi yangu ambayo ilifanya kama uchafu pale ndani. Sikujali!!!
“Utalala hapa ndani…na hawa watakuhudumia.” Nilipewa wakinamama wawili kwa ajili ya kunihudumia. Umri wao sidhani kama unatofauti sana na wa mwalimu Nchimbi yule mama yangu mzazi. Lakini matabasamu yao ni kama walikuwa na miaka kumi na nane.
Ungekuwa wewe ungejisikiaje. Mwenzako nilijisikia kama malkia.
Nilipata huduma zote za msingi hadi nilipopitiwa na usingizi na kuamka siku iliyofuata. Baada ya kuwa nimeoga na kupewa nguo nyingine nyeupe tena nilikaribishwa kifungua kinywa.
Ilikuwa kufuru nyingine tena niliyoweza kuishuhudia. Meza ilikuwa imesheheni kila aia ya makorokoro. Kazi kwako mlaji kujihudumia. Kiaibuaibu nikajinyima kula nilivyovitamani nikala nilivyovizoea. Na ushamba pia ulichangia. Kuna vyakula sikuelewa kama vinaliwa kwa kijiko ama uma, harufu yake nzuri ikabaki kunisurubu. Nikaogopa kujaribu!!!
Majira ya saa tano asubuhi niliongozwa tena kuelekea katika ile gari ya milango sita. Nikaingia humo kwa namna ileile kama malkia. Safari yetu ikaishia katika sehemu nyingine ya kifahari. Sikuwa naielewa nchi ya Zambia hivyo sikujua lolote.
“Mukuba Hotels.” Hilo ndilo neno nililoweza kulisoma baada ya kuunyanyua uso wangu juu. Sikujua maana ya Mukuba. Lakini bila shaka zilikuwa lugha za huko kwao. Hii hoteli ama jumba la kifal me!! Nilijiuliza.
SOMA HADITHI KAMILI HAPA>>>>>>>>>>>>>>>
Post a Comment