SITAISAHAU Facebook 5
https://menacotz.blogspot.com/2012/11/sitaisahau-facebook-5.html
MTUNZI: Emmy John P.
CONTCTS: 0654 960040
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA
“Isabella, Isabella….Jenipher jamani. Jenipher!!” “Amekuwaje tena. Eh!! Nambie.” “Jenipher yupo hoi hospitali hapa.” Alijitahidi kuongea bila taharuki lakini alisikika akitetemeka. Baada ya pale hata kabla sijamjibu, simu yake ilikatika. Nilipojaribu kumpigia hakupatikana. Nikajilazimisha kulala, huku nikiamini kuwa lile ni tatizo la kawaida tu Asubuhi palipopambazuka, Jenipher msichana aliyekuwa akiishi na huyo rafiki aliyenipigia usiku uliopita.alikuwa amefariki baada ya jitihada za madaktari kugonga mwamba. Ilikuwa habari ya kusikitisha sana kwani kilikuwa kifo cha ghafla mno. Sikuzikumbuka zile sauti za usiku ule zilikuwa zinasema nini na mimi. ‘Sitaisahau facebook!!” Je ni kazi hiyo pekee ya kulipwa milioni 6,666,000
ENDELEA
Mwili wa marehemu uliagwa katika viwanja vya Raila Odinga. Kila aliyehudhuria alijawa na simanzi, hasahasa kutokana na kilio cha mama mzazi wa binti yule ambaye alikuwa haishi kumlilia mwanaye huyo wa pekee aliyefanikiwa walau kufika chuo kikuu.
Tofauti na watu kuwa na majonzi niliweza kubaini sura ya mtu mmoja ilikuwa na hofu kuu. Huzuni ikiwa mbali naye.
Huyu alikuwa ni John. Sikujua kwa nini alikuwa katika hali ile. Niliyalaumu macho yangu kwa kumtazama vile huenda alikuwa sawa lakini hapana nafsi haikuridhika.
Muda wa kuaga ulifika ilianza familia ya marehemu iliyoungana nasi pale chuoni, kisha wakafuata wanafunzi wa kike. Nilinyanyuka na kuungana na msafara mrefu uliokuwa na nia moja ya kumsindikiza marehemu.
Jua kali lilikuwa likinisumbua sana na kunifanya nitokwe jasho sana, si mimi pekee niliyelalamika bali na baadhi ya wasichana waliokuwa nyuma yangu nao walilalamika. Lakini mwendokasi wa foleni haukuwa mbaya tuliamini kuwa muda si mrefu kila mmoja atakuwa amemuaga marehemu.
Kwa akili zangu timamu nilisikia mivumo kwa mbali sana. Sikuwa nimesinzia ili nijilaumu kwamba ni ndoto. Hapana nilikuwa najitambua kabisa. Mivumo ile ilikuwa mithili ya mkutano wa injili unaofanyika mbali kiasi na wanatumia spika kubwa kuhamasisha watu wengi waweze kusikia. Kisha sauti hizo kutwaliwa na upepo kish krudishwa. Sikuweza kusikia maneno yote na hata hayo niliyoyasikia yalikuwa nusunusu. Nilitaka kumuuliza aliyekuwa mbele yangu lakini bahati mbaya hatukuwa tukifahamiana. Lakini wa nyuma yangu nilikuwa namfahamu nikaamua kumuuliza kama kuna kitu anasikia.
“Eti dada unasikia nini?.” Nilimuuliza.
“Sijui hata kuna nini huko mbele hata dah!! Jua kali kweli.” Alinijibu nje kabisa ya swali nililomuuliza. Nikameza mate kulainisha koo langu, alikuwa amenikera.
Ghafla nikagundua kuwa foleni ile ilisimama, sasa nikagundua kwa nini yule binti alinijibu vile. Kumbe hakunielewa kabisa.
Kimyakimya nikamsamehe!!!
SOMA HADITHI KAMILI HAPA>>>>>>>>>
Post a Comment