FASTJET YAZINDUA MAUZO YA TIKETI ZA NDEGE ZA BEI POA ZAIDI TANZANIA


Ofisa Biashara Mkuu wa  Shirika la Ndege la Fastjet , Richard Bodin akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa mauzo ya tiketi za shirika hilo hapa nchini.
Wadau waliohudhuria uzinduzi huo
Mauzo ya tiketi ya fastjet yazinduliwa Tanzania
Nauli za chini zaidi kuwahi kutokea, watanzania wengi zaidi wanaweza kupaa

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKA la Ndege la kwanza  Afrika la nauli nafuu fastjet, leo limezindua mauzo ya tiketi zake nchini Tanzania, ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya kwanza ya kibiashara mwishoni mwa mwezi huu.

Uzinduzi wa tiketi hizo ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni hiyo kuwezesha usafiri wa ndege kwa watanzania, wako wengi ambao awali walikuwa hawamudu gharama za safari za ndege. 

Huku nauli za anga zikiwa zinaanzia Tsh32,000 (USD20) kabla ya kodi za serikali (VAT), usafiri wa anga sasa unakuwa moja ya njia nafuu za watu kusafiri.

Fastjet ambayo imeinunua FLY540, imechagua Dar es Salaam kuwa kituo chake cha kwanza cha uendeshaji Barani Afrika, huku safari za ndege zikiwa zimepangwa kuanza kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juluis Nyerere kuanzia Novemba 29. 

Tiketi za Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar-Mwanza zinaanza kuuzwa kuanzia leo. Safari zingi ne za ndani na Kanda ya Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada ya wiki kadhaa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winters amesema kuwa "Hiki ni kipindi cha kihistoria kwa safari za anga Tanzania na hasa Afrika. Usafiri wa anga siyo tena himaya ya watu wachache Tanzania. Fastjet itafanya usafiri wa anga kuwa kitu ambacho watanzania wengi wanakimudu tofauti na awali, hivyo kutoa fursa nzuri kwa zaodo kwa wafanyabiashara, safari za likizo na wanafamilia  kutembeleana".

Tiketi zinapatikana kupitia mawakala wa usafiri wa na dawati la mauzo, kituo cha mawasiliano na ofisi za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet, www.fasthet.com itazinduliwa wiju ijayo na kutoa taarufa za safari na nauli. Tovuti hiyo pia itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za credit/debit pamoja na simu za mkononi.

Related

MATUKIO 1724873713759874038

Post a Comment

1 comment

Anonymous said...

I love reading through a post that can make men and women think.
Also, thank you for allowing me to comment!
Also visit my webpage :: perfumes

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item