FASTJET YAZINDUA MAUZO YA TIKETI ZA NDEGE ZA BEI POA ZAIDI TANZANIA
https://menacotz.blogspot.com/2012/11/fastjet-yazindua-mauzo-ya-tiketi-za.html
Ofisa
Biashara Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet , Richard Bodin
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam kuhusu uzinduzi wa mauzo ya tiketi za shirika hilo hapa nchini.
Wadau waliohudhuria uzinduzi huo
Mauzo ya tiketi ya fastjet yazinduliwa Tanzania
Nauli za chini zaidi kuwahi kutokea, watanzania wengi zaidi wanaweza kupaa
DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKA la Ndege
la kwanza Afrika la nauli nafuu fastjet, leo limezindua mauzo ya
tiketi zake nchini Tanzania, ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya
kwanza ya kibiashara mwishoni mwa mwezi huu.
Uzinduzi wa
tiketi hizo ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni hiyo kuwezesha
usafiri wa ndege kwa watanzania, wako wengi ambao awali walikuwa
hawamudu gharama za safari za ndege.
Huku nauli za
anga zikiwa zinaanzia Tsh32,000 (USD20) kabla ya kodi za serikali (VAT),
usafiri wa anga sasa unakuwa moja ya njia nafuu za watu kusafiri.
Fastjet ambayo
imeinunua FLY540, imechagua Dar es Salaam kuwa kituo chake cha kwanza
cha uendeshaji Barani Afrika, huku safari za ndege zikiwa zimepangwa
kuanza kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juluis Nyerere kuanzia
Novemba 29.
Tiketi za Dar es
Salaam-Kilimanjaro na Dar-Mwanza zinaanza kuuzwa kuanzia leo. Safari
zingi ne za ndani na Kanda ya Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada ya
wiki kadhaa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winters
amesema kuwa "Hiki ni kipindi cha kihistoria kwa safari za anga Tanzania
na hasa Afrika. Usafiri wa anga siyo tena himaya ya watu wachache
Tanzania. Fastjet itafanya usafiri wa anga kuwa kitu ambacho watanzania
wengi wanakimudu tofauti na awali, hivyo kutoa fursa nzuri kwa zaodo kwa
wafanyabiashara, safari za likizo na wanafamilia kutembeleana".
Tiketi
zinapatikana kupitia mawakala wa usafiri wa na dawati la mauzo, kituo
cha mawasiliano na ofisi za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet,
www.fasthet.com itazinduliwa wiju ijayo na kutoa taarufa za safari na
nauli. Tovuti hiyo pia itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za
credit/debit pamoja na simu za mkononi.
1 comment
I love reading through a post that can make men and women think.
Also, thank you for allowing me to comment!
Also visit my webpage :: perfumes
Post a Comment