KADINALI PENGO AZUNGUMZIA KUPIGWA RISASI PADRI ZANZABAR.
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/kadinali-pengo-azungumzia-kupigwa_2.html
Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
ASKOFU
wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kadinali Pengo amelaani kitendo cha kupigwa risasi kwa Padri wa kanisa
hilo, Parokia ya Mpendaye mjini Zanzibar, Ambrose Mkenda na kusema
kitendo hicho hakileti matumaini mema kwa amani ya nchi katika siku za
usoni.
Desemba
24 mwaka 2012, Padri Mkenda alipigwa risasi na watu wasiofahamika nje
ya nyumba yake na kufikishwa katika Hospitali ya Muhimbili ambako
alitolewa risasi mbili.
Jana, Pengo akizungumza katika ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam, alisema tukio hilo na vurugu za kuchomwa makanisa ni ushahidi wa wazi kuwa watu hawaitaka amani nchini.
Jana, Pengo akizungumza katika ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam, alisema tukio hilo na vurugu za kuchomwa makanisa ni ushahidi wa wazi kuwa watu hawaitaka amani nchini.
“Padri
wetu Zanzibar wakati anapigwa risasi hakuwa anatoka kwenye vilabu vya
pombe wala hakuwa katika majumba ya watu, alikuwa anatoka kutimiza
majukumu yake ya kiuchungaji lakini akapigwa risasi nje ya nyumba yake,
tunakwenda wapi?” alihoji Pengo.
Kadinali Pengo alisema vurugu za kidini zinazoendelea kujitokeza nchini hivi sasa hazileti dalili njema kwa amani ya nchi.
Kadinali Pengo alisema vurugu za kidini zinazoendelea kujitokeza nchini hivi sasa hazileti dalili njema kwa amani ya nchi.
“Hata
hao wanaofikiri kuwa wakibaki pekee yao na dini zao watakuwa salama
hawapo sahihi kwani kuna nchi hivi sasa zipo katika vurugu ingawa zina
imani moja ya dini,” alisema Pengo.
Alisema, “Angalieni nchi kama Tunisia, Algeria na nchi nyiingine hazipo salama ingawa zina imani moja ya dini.”
Alisema, “Angalieni nchi kama Tunisia, Algeria na nchi nyiingine hazipo salama ingawa zina imani moja ya dini.”
Alisema
wanaochochea vurugu za kidini watambue kuwa hata kama dini nyingine
itaondoka na wao kubaki pekee yao hawatabaki salama.
Kadinali
Pengo aliwataka Watanzania kuwa macho na tofauti ambazo zinaweza kuleta
vifo katika jamii kwani tofauti za kidini zisiwe sababu ya kutukanana,
kukashifiana kwani dini zote zinatoka kwa baba mmoja hivyo haoni sababu
za kujengeana chuki.
Pengo
alisema mamlaka ya Serikali siyo kusimamia msingi wa dini yoyote na
inachaguliwa na watu wote hivyo kazi yake ni kuwahakikishia watu wa dini
zote usalama wao na mali zao na iwapo itashindwa na kuwabagua watu
kulingana na imani zao ni wazi kuwa itakuwa imepoteza mwelekeo.
“Watu
wa imani zote za dini wanapaswa kulindwa na Watanzania wametakiwa
kuliombea Taifa lao ili liweze kudumu katika imani na mataifa mengine
yaweze kuiga kutoka kwetu,” alisema Pengo na kuongeza kuwa Taifa
linahitaji maombi zaidi kipindi hiki kuliko wakati mwingine.
Padri
huyo alitolewa risasi mbili kinywani na hali yake inaendelea vizuri na
hadi juzi kulingana na taarifa za Jeshi la Polisi Zanzibar, watu wawili
walikuwa wakishikiliwa na jeshi hilo kuhusiana na shambulizi hilo na
katika ghasia zilisababisha kuchomwa kwa makanisa Zanzibar na Dar es
Salaam watu kadhaa kesi zao zipo mahakamani
Post a Comment