TAARIFA YA .MAUAJI YA KUTISHA- MBEYA
https://menacotz.blogspot.com/2013/01/taarifa-ya-mauaji-ya-kutisha-mbeya.html
WILAYA YA MOMBA – MAUAJI
MNAMO TAREHE 13.01.2013 MAJIRA YA
SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KALUNGU KIJIJI CHA IVUNA TARAFA
YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. WATU WAWILI AMBAO NI 1.ERNEST
S/O TWINI MOLELA NA MIZINARA D/O MILILO @ MATELA WOTE WAKAZI WA KIJIJI
CHA IVUNA WALIUAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUWAZIKA
KATIKA KABURI MOJA .
CHANZO NI TUHUMA ZA KISHIRIKINA
BAADA YA MAREHEMU HAO KUTUHUMIWA KUWA NI WACHAWI KWA KUMLOGA MAREHEMU
NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 12.01.2013 MAJIRA YA
SA 16:00HRS BAADA YA KUUGUA MUDA MREFU. TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI WA
MAZISHI YA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA AMBAPO KUNDI LA WATU
WASIOPUNGUA KUMI WALIPANDISHA HASIRA NA KUWATUHUMU MAREHEMU HAO KUHUSIKA
NA KIFO CHA NDUGU YAO NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA HIVYO KUANZA
KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA NGUMI, FIMBO NA MAWE KISHA KUWATUMBUKIZA
KATIKA KABURI ALILOKUWA AKIZIKWA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA
WAKIWA HAI NA KUWAZIKA WOTE WATATU KATIKA KABURI HILO MOJA.
BAADA YA HAPO WATU HAO WALIKWENDA
NYUMBANI KWA ERNEST S/O TWINI MOLELA NA KUICHOMA MOTO NYUMBA YAKE.
KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA WAWILI WALIOKUWA VINARA WA TUKIO HILO
WAMEKAMATWA AMBAO NI 1. VENA S/O ERNEST MOLELA [MTOTO WA MAREHEMU ERNEST
S/O TWINI MOLELA], MIAKA 26, MUWANDA, MKULIMA NA 2. EMANUEL S/O
CHRISTOPHA, MIAKA 16, MUWANDA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA.
MAREHEMU WOTE WATATU NI NDUGU WA UKOO MMOJA. TARATIBU ZA KUFUKUA KABURI
ILI MIILI YA MAREHEMU IFANYIWE UCHUNGUZI ZINAFANYWA. AIDHA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE
WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA. PIA ANAIASA JAMII
KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII
IKIWA NI PAMOJA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO. AIDHA ANATOA RAI KWA
JAMII/KIKUNDI CHA WATU WENYE KERO/MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE MAALUM
KUTAFUTA NJIA ILIYO HALALI KUFIKISHA KERO,MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE WAO
KWA NJIA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUTUMIA VURUGU/FUJO NA KUSABABISHA
MAUAJI.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 13.01.2013 MAJIRA YA
SAA 17:25HRS HUKO MLIMA MBALIZI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. GARI T. 403 AAP / T.448 AXN AINA YA SCANIA
SEMI TRAILER LIKIENDESHWA NA DEREVA FILSON S/O EDSON,MIAKA 32,MUWANJI
MKAZI WA DSM LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI T.841 CDJ AINA YA SHANREY
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA BECKSON S/O BEBEZERI,MIAKA 66,KYUSA,MKULIMA
MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO . MTUHUMIWA
AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDESHA PIKIPIKI
KUTAKA KUYAPITA MAGARI YALIYOKUWA MBELE YAKE. UCHUNGUZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment