ZIARA YA JK TABORA: NASSOR WAZAMBI ATOA MAWAZO KUPITIA FACEBOOK

JK aanza ziara ya siku 4 mkoani Tabora.

Leo kaanzia Igunga na atatembelea wilaya zote 7 kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

BARABARA
katika hali ya kushangaza Wachina wanao tengeneza barabara za Tabora ->itigi, Nzega -> puge, Tabora -> puge na wale wa Tabora -> urambo, speed yao imeongezeka ghafla na njia zao za diversion zikiwa zimeboreshwa.

KITETE HOSPITAL
kitete hospital dawa za kumwaga, ma ward ni masafi kuliko huku vitanda vikiwa vimetandikwa shuka mpya! na kila wodi kumefungwa Tv flat screen mpyaa, mbona raha.
USAFI WA MJI.
mji wa Tabora hali ya usafi imeboreshwa kwa kiwango cha juu, magari ya kuzoa taka yote yamepona, taka kwenye makontena zina mwagwa kwa wakati, nyasi pembeni ya barabara zina fyekwa karibu kila siku, mifereji imezibuliwa. hongera meya Gulam Dewji teh teh

BODABODA
Kamata kamata ya bodaboda iliyokuwa imeanza chini ya SUMATRA na Police imesimamishwa kwa muda mpaka tarehe 10 siku ambayo JK ataondoka, angalau vijana watapumua kwa muda mwee!

KARIBU TABORA MJUKUU WETU Jakaya Mrisho Kikwete sikunyingine uwe unakuja ghafla ufurahi na roho yako.
HAHAHAHAHA
bhangi bhulya bhangi...

Related

WAZAMBI 8581498500899013503

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item