KAMATI YA UCHAGUZI NI MADUDU MTUPU-SHAFIH DAUDA

HUU NDIO UKWELI WA KUENGULIWA KWA SHAFFIH DAUDA KTK UCHAGUZI WA TFF - NA MADUDU MENGINE YA KAMATI YA UCHGUZI


Februari, 2013 Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitoa majina ya wagombea waliopitishwa kuwania uongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya TFF na Bodi ya Ligi Kuu ya Bara.

Katika majina hayo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, ambaye ni mchumi aliyebobea, yapo majina ya wagombe ambao wamekatwa kuwania uongozi katika TFF kutokana na sababu mbalimbali ambazo hata hivyo, mtandao huu unaona bado kuna maswali mengi ya kujiuliza kutokana na uamuzi wa kamati hiyo.

Hapa chini baadhi ya maamuzi ya kutatanisha juu ya kamati hiyo, inayoongoza na mwanasheria aliyebobea, Lyatto.

Kwa mfano;

Shafii Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.

Mantiki:

Kwa mujibu wa kamati hiyo, Dauda amebainika hana sifa za kugombea uongozi TFF kutokana na kutokidhi Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwamba, ameonekana kuwa kwa kuwa si mkweli, alipotosha umma na hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF.

Kwa kuwa si mkweli – Kwa mujibu wa kamati ya uchaguzi, Dauda anaonekana si mkweli hasa baada ya kushindwa nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa DRFA pale aliposema uchaguzi huo haukuwa huru na haki kwani wapiga kura wake walionekana wakipokea maelekezo ya nani wa kumpigia kura kutoka kwa kiongozi mmoja wa DRFA.

Alipotosha umma – Kamati inadai, Dauda mara baada ya kushindwa katika uchaguzi wa DRFA alidanganya umma kuhusu ushiriki wake kwa kusema, alikwenda kushiriki kwa kazi maalum ya kubaini madudu yanayoendelea ndani ya chaguzi za vyama vya soka. Hayo aliyasema kupitia kipindi cha michezo cha Sports Xtra kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Clouds FM ambacho Dauda ni mwajiriwa.

Hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF- Kama inavyojieleza, kamati imesema Dauda hana ufahamu wowote juu ya katiba ya TFF ambayo ipo katika ofisi za shirikisho hilo Ilala jijini Dar es Salaam.

Ukweli wa mambo;

Kwa kuwa si mkweli- Si kweli kamba Dauda hakuwa mkweli kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA kwani kila kitu kilikuwa wazi, umma mzima wa Watanzania uliona kupitia luninga namna wapiga kura wa DRFA walivyokuwa wakipokea maagizo ya nani wa kumpigia kura ndani ya ukumbi kulikofanyika uchaguzi huo kitendo ambacho si halali huku muda wa kampeni ukiwa umekwisha. Hapo ushahidi wa sauti na picha upo, Je, uongo wa Dauda umetoka wapi. Kamati ilipaswa kutafuta ushahidi huo kwa njia inazojua ili kubaini uongo wa Dauda. Yawezekana wazi kwamba, kamati ilihofu Dauda anaweza kufichua mambo mengi zaidi endapo ataruhusiwa kuingia katika chumba cha mkutano wa TFF.

Alipotosha umma – Inaweza kuwa kweli Dauda alitamka kwamba alienda kugombea uongozi DRFA kwa kazi maalum, lakini halikuwa tamko rasmi la kituo cha redio au mgombea binafsi. Lazima vitu viwili vitenganishwe hapa, kwamba Dauda mfanyakazi wa Clouds na Dauda mgombea wa DRFA, hawa ni watu wawili tofauti. Kama mgombea wa DRFA, Dauda hakupotosha umma na hata akiwa mfanyakazi wa Clouds, hana kosa alilofanya juu ya kauli hiyo isiyo rasmi.

Hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF - Si kweli kwamba Dauda hana ufahamu wa katiba ya TFF, katika usaili aliulizwa kuhusu kazi ya kamati ya utendaji naye alijibu kwa ufasaha lakini kamati ya uchaguzi ilitaka ataje kazi hizo katika mlolongo kama ulivyoandikwa katika katiba hiyo. Yawezekana kamati ilitaka Dauda awe amekariri katiba hiyo kama masomo mengine ya darasani tena wale wa shule ya msingi. Ajabu ni kwamba, wagombea wengine wa nafasi aliyoomba Dauda hakukumbana na swali hilo.

MSIMAMO WA MTANDAO HUU;

Inaonekana wazi uongozi ndani ya TFF hautaki kuingiza sura ngeni na tayari mfumo umewekwa kuhakikisha viongozi ndani ya taasisi hiyo wawe wametokana na TFF yenyewe, MTU MPYA hatakiwi ndani ya TFF.



Tazama zengwe lingine;

Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.

Ukweli na haki;

Baada ya kuenguliwa katika uchaguzi wa FRAT, Abdulkadir alitumia haki ya msingi ili kupata haki yake, hilo ni kosa kwa TFF na moja kwa moja imemtosa katika uchaguzi huu. Walichotaka TFF ni kwamba, Abdulkadir hata kama aliona hakutendewa haki katika uchaguzi wa FRAT angekaa kimya ili matakwa ya baadhi ya watu yatimie.



Hii ndiyo aibu nayo;

Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba.

Ilivyokuwa;

Mvella ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF akiwakilisha mikoa ya Mbeya na Iringa, sasa katika ule mchakato wa TFF kutaka kubadilisha katiba, yeye alikataa kukubaliana na wajumbe wenzake wa kamati ya tendaji. Mtu kutetea haki yake na maslahi ya soka Tanzania, ameondolewa kuwania uongozi TFF.

Kamati ya uchaguzi ya TFF ilitaka Mvella akubali kila kitu kutoka TFF ili mambo ya baadhi ya watu yaweze kwenda. Hii si haki.

MSIMAMO WA MTANDAO HUU;

Abdulkadir na Mvella wameonyesha wao ni watu makini pia ni wawakilishi wa kweli kwa watu wao, lakini kwa kuwa ni wabishi wa kutaka kupelekwa pelekwa tu na TFF wameondolewa katika mchakato wa uchaguzi. Hii ina maana, ukiwa ndani au nje ya TFF unatakiwa kukubali kila kitu kinachotoka au kusemwa na TFF jambo ambalo si sahihi katika nchi ya demokrasia kama Tanzania na hata katiba ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) haielekezi hivyo.

Tunaamini kwa kuwa kamati ya uchaguzi ina watu makini inawezaaa kupitia upya uamuzi huu muda mfupi tu baada ya wagombea hawa walioenguliwa watakapokata rufaa kama wakiona kuna haja ya kufanya hivyo.
hhh 

Related

UCHAGUZI 7834875432397857711

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item