DK.SLAA ALAANI YALIYOTOKEA BUNGENI

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr.Willbrod Slaa amefanya mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema
1. CHADEMA Inalaani uonevu na uvunjwaji wa Kanuni unaofanywa na kiti cha Spika
2. Hoja zote za CHADEMA zilizokataliwa Bungeni zitapelekwa kwenye mahakama kubwa kuliko zote nayo ni MAHAKAMA YA UMMA
3. Hakuna Mbunge yoyote wa CHADEMA akayeenda kuhojiwa na kamati Uongozi ya maadili ya Bunge mpaka hapo rufaa zote zaidi ya 10 za Wabunge wa CHADEMA dhidi ya maamuzi ya kiti cha Spika zitakapojibiwa
4. Ni aibu kwamba Bunge la sasa halina rejesta ya maamuzi ya Spika kama ilivyo kwa Mabunge mengine ya Jumuiya ya Madola hali inayomfanya Spika na Naibu wake kujiamulia mambo kienyeji tu bila kufuata Kanuni za Bunge na bila kuweka rekodi ya maamuzi yao kwenye hoja mbalimbali.
5. CHADEMA haitakubali dhuluma wala uonevu wowote mwaka huu kwani mwaka huu ni mwaka wa NGUVU YA UMMA

kwa taarifa zaidi angalia video hii hapa chini

Related

RAIS BANDA AWAFUKUZA MAWAZIRI WAKE WOTE KWA UFISADI

Rais wa Malawi, Joyce Banda amelifuta kazi baraza lake la mawaziri kutokana na kuongezeka kwa visa vya ufisadi serikalini. Maafisa wa serikali wamekuwa wakipatikana na pesa zikiwa zimefichwa chini ya ...

ZITO AMSIFIA KIKWETE

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema Rais Jakaya Kikwete ni mtu wa ajabu na kueleza kuwa kama si uvumilivu wake nchi ingekuwa katika machafuko makubwa. Zitto ametoa kauli hiyo ju...

MBOWE NA ZITTO WAUNGURUMA TABORA

>> MBOWE ASEMA HAWATAMPOKEA KIONGOZI ALIYEFUKUZWA CCM  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw.Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa ndani wa chama hicho wa...

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in weekRecentBLOG ZINGINE

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item