UEFA CHAMPIONZ LIGI: DUNIA KUTIKISIKA REAL v MAN UNITED JUMATANO USIKU!

>>MOURINHO ADAI: ‘DUNIA NZIMA INANGOJEA MECHI HII!’  

>>MARA YA MWISHO MOURINHO v FERGIE ni INTER v UNITED, 0-0 & 0-2!!

FERGIE_n_MOURINHOMENEJA MACHACHARI wa Real Madrid Jose Mourinho amedai Dunia nzima inalingojea pambano la Timu yake na Manchester United litakalochezwa Uwanjani Santiago Bernabeu Jumatano Usiku ikiwa ni Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Timu hizi zitarudiana Uwanjani Old Trafford hapo Machi 5.
Mourinho, aliekuwepo Uwanjani Old Trafford kuishuhudia Man United ikiichapa Everton Bao 2-0 hapo jana na kupaa kileleni mwa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 12 mbele ya Timu ya Pili Man City, alisema: “Hii ni Mechi ambayo Dunia nzima inaingojea. Dunia haisubiri kuona Timu nyingine, natumaini tutaipa Dunia utamu tu!”
Mourinho pia alizungumzia Urafiki wake na Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson na kusema: “Nasikia fahari na bahati kwa sababu huyu ni Mtu muhimu katika Dunia ya Soka na, juu zaidi, ni Mtu mwema. Siku zote nimekuwa na uhusiano mzuri na yeye na hili linanipa fahari. Tumekuwa na Mechi nyingi kati yetu kuanzia nipo Porto. Nikaenda Chelsea, Inter na sasa Real. Kote nimekutana na Sir Alex. Ndio nataka kushinda lakini naamini yeyote atakaefungwa ataridhika na kupumua kirahisi kwa sababu ya urafiki wetu!”
+++++++++++++++++++
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumanne 12  Februari 2013
Celtic v Juventus
Valencia v Paris St Germain
Jumatano 13  Februari 2013
Real Madrid v Manchester United
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
+++++++++++++++++++
HISTORIA
Real Madrid na Manchester United hawajakutana kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu Robo Fainali ya Mwaka 2003 ambayo Real walishinda kwa jumla ya Mabao 6-5 baada ya kushinda Mechi ya kwanza 3-1 huko Santiago Bernabeu na kufungwa 4-3 Uwanjani Old Trafford huko Ronaldo de Lima akapiga Hetitriki.
Mbali ya pambano kuwa zito, Mechi hii itakuwa na mvuto kwani Cristiano Ronaldo atarudi Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aihame Man United na kwenda Real Madrid Juni 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 80.
+++++++++++++++++++
Man United v Real Madrid
-1957: European Cup-Nusu Fainali: Real washinda 3-1Madrid, sare 2-2 na Real kushinda Jumla ya Bao 5-3
-1968: European Cup-Nusu Fainali: Man United washinda 1-0 Old Trafford, sare 3-3 ugenini na Man United washindi Jumla ya Bao 4-3
-2000: European Cup-Robo Fainali: Sare 0-0 huko Bernabeu, Man United wafungwa 3-2 nyumbani
-2003: European Cup-Robo Fainali: Real washinda 3-1 nyumbani, Man United washinda 4-3 nyumbani, Real wapita Jumla ya Mabao 6-5.
+++++++++++++++++++
Mara ya mwisho kwa Sir Alex Ferguson kumvaa Jose Mourinho ilikuwa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2009 wakati Man United ilipoibwaga Inter Milan kwenye Robo Fainali baada ya kutoka 0-0 na kuifunga 2-0 Old Trafford kwa Bao za Vidic na Ronaldo.
Ferguson amesema: “Ni nafasi nzuri kwa Mashabiki wetu kumuona Ronaldo tena na mimi kukutana na Jose-itabidi niagize Mvinyo safi!”
+++++++++++++++++++
RATIBA-MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumanne 19  Februari 2013
Arsenal v Bayern Munich
FC Porto v Malaga
Jumatano 20  Februari 2013
Galatasaray v FC Schalke
AC Milan v Barcelona
MARUDIANO
Jumanne 5 Machi 2013
Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk
Man United v Real Madrid
Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic
Paris St George v Valencia
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
+++++++++++++++++++

Related

UEFA 8182507404079944021

Post a Comment

ads by blogger

Follow Us

Hot in week

BLOG ZINGINE

BLOG OWNER

BLOG OWNER
MESHACK JACKSON

Side Ads

Instagram

JOIN US ON TWITTER

Text Widget

Millard Ayo – Official Website

item